Na Amini Nyaungo
Timu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Mkoani Dodoma ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo imeshinda magoli 2-0 dhidi ya timu ya RAS ya mkoa wa Singida katika mchezo wa mpira wa miguu uliopigwa leo katika dimba la Bombadia Mkoani Singida leo Januari 04.2025.
Bonanza hilo la Michezo lilijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Kukimbia na Magunia, Mchezo wa Bao, Karata, Mchezo wa Wavu, Mashindano ya Kula ambapo limefanyika katima uwanja wa Bombadia Mkoani hapa ikiwa na lengo la kukuza ushirikiano na uhusiano kazini, kuchangia maendeleo ya kiuchumi hususani kwa Mkoa wa Singida ambao wamekua waenyeji wa bonanza hilo.
Akizungumza wakati wa bonanza Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaudi Kigahe amesema kuwa wameuchagua mkoa wa Singida kuwa waenyeji wa bonanza hilo kwa sababu mbalimbali kama vile uwepo wake kati kati ya nchi, ukuaji wake katika sekta ya viwanda vidogo na vikubwa ambapo watatumia fursa hiyo kukuza na kuboresha maeneo ya ufanyaji biashara kwa kuzungumza na wafanyabaishara mbali mbali wa mkoani Singida.Bonanza hilo limefanyika leo Januari 04,2025 katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida ambapo mgeni Rasmi katika Bonanza hilo akiwa ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (Mb) ambapo amefungua bonanza hilo.
Ikiwa na kauli mbinu ya Bonanza hilo ni "Michezo Huongeza Ufanisi Mahala pa Kazi Shiriki Michezo Jenga Afya Yako".Malengo ya Bonanza hilo ikiwa ni pamoja na kukuza uhusiano na ushirikiano miongoni mwa watumishi kusaidiana na Kushirikiana, Kuchangia katika kukuza uchumi Mkoani hapo, Kuibua vipaji kwa vijana na washiriki,Uchangiaji Damu na kupima Afya Bure.
Mwisho

Post a Comment