IGHONDO APONGEZA MIRADI NA KUIKATAA MINGINE

 Na Amini Nyaungo

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo jana Januari 02,2025 amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotokana na fedha za mfuko wa jimbo la Singida Kaskazini yenye thamani ya shilingi milioni themanini na nne laki sita na sitini.

Katika Ziara hiyo Ighondo amepongeza maendeleo na matumizi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya maendeleo ya miradi hiyo,  ambapo amewapongeza wasimamizi  wa mradi wa nyumba ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Mangida ambapo imetolewa shilingi milion 11 kutoka katika mfuko wa Jimbo.


"Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mliyoifanya hapa hata mkituambia nataka kumalizia itakuwa rahisi kupata tena,"Ighondo


Aidha Mbunge huyo amewataka wananchi wa eneo hilo ushirikiano katika mambo mablimbali ya maendeleo.
"Naomba tuendelee kushirikiana katika hali yoyote naamini tutafanya vizuri zaidi na zaidi," amesema

Licha ya kutoa pongezi kuna baadhi ya miradi hakukubali kutokana na kutotumika vizuri fedha ambazo zimeombwa kwa ajili ya maendeleo.


Ighondo ameukataa mradi wa fedha za Jimbo wa shule shikizi iliyopo Itaja mkoani hapa ambapo kiasi cha shilingi milioni mbili imetolewa lakini matumizi yake hayajaenda vizuri.

"Sikubaliani na huu mradi hapa unaona kabisa hii sio sahihi naomba kupata maandishi," Ighondo

Mradi mwingine uliokataliwa ni pamoja na Shule ya msingi Munkhola iliyopo kata ya Mgori ambapo mfuko wa Jimbo kutoka kwa Mbunge umetoa kiashi cha shilingi laki tano na wamepaua chumba kimoja tu ambapo hakija kamilika.
Mbunge huyo ameomba kupata taarifa za maandishi katika miradi yote aliyopita kwa ajili ya kupiga mahesabu vizuri akisema kuwa pesa zilizotumika ni za serikali hivyo wataangalia kila sehemu kubaini wapi kumekaa sawa na wapi kuna mapungufu.

"Niwakumbushe tu kuwa nahitaji maandishi manunuzi na matumizi ya fedha zilizotoka katika mfuko wa Jimbo," Ameongeza
Katika Msafari huo umejumuisha wanakamati ya mfuko wa Jimbo  la Singida Kaskazini ambao kwa pamoja wameridhia matumizi ya fedha ya miradi hiyo.

Katibu wa Kamati ya mfuko wa Jimbo lakini pia ndiye Afisa Mipango Wilaya ya Singida Vijijini Elia Simanjilo amesisitiza kila mmoja aliyepitiwa na kupata fedha za miradi basi atawajibika kutoa taarifa ya manunuzi na matumizi.

Lakini pia ameridhishwa na maeneo mengi walivyoweza kuwekeza katika ujenzi wa miradi.
Isack Timothy yeye ni Mjumbe wa Kamati hiyo pamoja na Bebora Ituka kwa pamoja wamewashauri watendaji na viongozi mbalimbali wanapopata pesa basii wazielekeze katika lengo lililokusuidiwa.
Naye Afisa Utumishi Msaidizi wa Wilaya ya Singida Vijijini Magreth Magasha alikuwepo katika msafara yeye amehaidi changamoto za baadhi ya watumishi kukosekanna amelichukua na kulipeleka sehemu husika ili kama wapo basi wapatiwe na waanze kazi.

"Nimesikia changamoto ya Watumishi niwaahidi nimechukua na nitafanyiakazi kwa kupeleka sehemu husika," Magreth.

Moja ya maeneo ya miradi waliyoitembelea ni pamoja na Madamigha wakiwa na mradi wenye thamani ya  milioni nne na   laki saba themanini(Ofisi ya Kijji cha Madamigha)
Lakini pia wametembelea katika Zahanati ya Makhandi iliyokuwa na mradi wenye thamani ya Milioni 5 kwa ajili ya kununua Fenicha.
Msafara huo pia umetembelea MITULA mradi una thamani wa milioni tatu na laki tatu na elf ishirini ili  kukamilisha nyumba ya mwalimu ambapo wanakaa walimu wawili na mradi huu wameukubali walitembelea Shule shikizi ya Mvae mradi wa milion kumi katika shule shikizi kata ya Merya.

Pia  Maghojoa wamepata milioni sita kwa ajiri ya ujenzi, Zahanati ya Mwachambia,  Mangida jengo la walimu lenye thamani ya milioni tatu hii ni baadhi ya miradi ambayo imetembelewa kati ya mingi hapo jana.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post