Na Amini Nyaungo
Mkoa wa Singida umepokea vifaa vya usafiri vyenye thamani ya shilingi milioni mia moja na sabini na nane na laki sita kwa ajili ya kuhudumia maswala ya Afya na chanjo.Vifaa hivyo ni gari moja aina ya Canter na Pikipiki kumi na moja (11) ambavyo vimepokelewa leo (Januari 11,2025) na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ofisini kwake mkoani hapa.
Baada ya kupokea vifaa hivyo Dendego amesema kuwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan anaendelea kujali afya za wananchi wake kwa kutoa usafiri ambao utasaidia kuwafikia kwa haraka.
Aidha, Dendego amesema kuwa gari hiyo pamoja na Pikipiki zimeleekezwa katika huduma ya chanjo ambapo Mkoa wa Singida uliongoza kwa utoaji wa chanjo katika mikoa yote Tanzania.
"Rais Samia anaendelea kuupiga mwingi kwani ameleta vifaa vya usafiri kwa ajili ya huduma ya chanjo hii itatusaidia kufika kwa haraka na kutoa huduma bora," Dendego.Mwisho.
Post a Comment