Na Amini Nyaungo
MKUU wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, amewataka viongozi na wakandarasi kusimamia vyema miundombinu ya barabara ili ziweze kuwa bora kutumika muda mrefu na zisaidie kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Singida huku akiwataka wasimamizi kuwa makini na usafi wa barabara.Hayo ameyasema leo (Januari 15,2025) katika kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida akiwa na wajumbe wa kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na kuwataka wawe makini wanapoisimamia miradi yote ili kuifanya Singida kuwa sehemu salama na mipango ya kuelekea kuwa jiji.
Katika hotuba yake Dendego ametaka Barabara za Singida kuwa kama nchi ya Dubai au Singapore kwa uzuri lakini pia amempongeza Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika taifa la Tanzania kwa kuleta fedha nyingi za maendeleo mkoa wa Singida.
" Naomba kwa niaba yenu kutoa shukrani za dhati kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali anayoiongoza ya Awamu ya Sita kwa kutuletea fedha nyingi mwaka uliopita na kutenga fedha nyingi mwaka huu kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ikiwemo barabara, madaraja, vivuko, makaravati ili kuwezesha wananchi wetu kusafiri na kusafirisha mizigo yao kutoka pande zote za Mkoa wa Singida,"DendegoAidha, Dendego amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa uliidhinishiwa jumla ya Sh. Bilioni 49.4 ambapo TANROADS Sh. Bilioni 24.9 na TARURA Sh. Bilioni 24.5 hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2024 TANROADS walipokea Sh. Bilioni 8.3 na TARURA Sh. Bilioni 12.4.
Kwa mwaka 2024/2025 Mkoa wa Singida umetengewa jumla ya Sh. Bilioni 48.2 ambapo TANROADS wameidhinishiwa Sh. Bilioni 19.1 na TARURA Sh.
Bilioni 29.1.
Katika hatua nyingine Dendego amesema kuwa kazi kubwa zilizofanyika kwa kipindi hiki cha miaka mitatu (3) ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na kuongeza kilometa za lami kutoka 499.28 hadi 543.09 (ongezeko likiwa ni kilometa 43.81, Kuongeza kilometa za changarawe kutoka kilometa 1,870.81 mwaka 2021 hadi kilometa 3,118.59 mwaka 2024/2025, Kukamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 27, madogo 1,638, culverts 2,341 na vivuko 65." Hali hii imefanya barabara zetu ziweze kupitika mwaka mzima toka asilimia 78 hadi asilimia 82.8," Dendego
katika kuhakikisha mirqdu hii ya maendeleo inaendelea kudumu kwa muda mrefu Mheshimiwa Dendego amesema kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuilinda na kuiheshimu.
" Wajibu wetu mkubwa ni kulinda miundombinu hiyo na kuhakikisha muda wote panapotokea uharibifu kwa sababu yeyote ile tunafanya matengenezo/ukarabati mara moja. Na iwapo uharibifu huo utasababishwa na uzembe au matendo yasiyofaa ya binadamu kama, Kung’oa vyuma, Kumwaga mafuta barabarani, Ajali za kizembe, Kupitisha mifugo na nyinginezo hatua kali zichukuliwe dhidi ya waharibifu hao," Dendego
Mwisho
Post a Comment