Na Amini Nyaungo
Kuchelewa kwa fedha za baadhi ya miradi ya maendeleo kumetokana na serikali kushughulikia na kuipa kipaumbele miradi mikubwa ambayo ilikuwa inafikia hatua ya mwisho ya ukamilishaji wake.
Katika hatua nyingine Dokta Mwigulu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kugawa fedha za maendeleo ili kuwafanya wananchi wake waishi katika matumaini na maendeleo.
Kuchelewa kwa fedha za baadhi ya miradi ya maendeleo kumetokana na serikali kushughulikia na kuipa kipaumbele miradi mikubwa ambayo ilikuwa inafikia hatua ya mwisho ya ukamilishaji wake.Hayo ameyasema leo (Januari 15,2025) Waziri wa Fedha Daktari Mwigulu Lameck Nchemba katika kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida ambacho Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.
Dk.Mwigulu amesema kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere lililopo Rufuji Mkoani Pwani ambapo faida na matokeo yake hivi sasa umeme unapatikana vizuri pia ukamilishaji wa daraja la Magufuli la Busisi Kigongo lililopo Mwanza pamoja na reli ya kisasa ya mwendokasi ya SGR.
Aidha, amesema kuwa baada ya miradi hiyo kufikia pazuri hivi sasa fedha za miradi mbalimbai za maendeleo zinakuja mikoa yote ikiwemo kwa ajili ya barabara, Zahanati, Shule na sehemu nyingine za maendelo.
"Baada ya miradi ile kukamilika basi sasa fedha za maendeleo zitakuja na zitaendelea kutumika katika maeneo yaliyoelekezwa,''Mwigulu.
Katika hatua nyingine Dokta Mwigulu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kugawa fedha za maendeleo ili kuwafanya wananchi wake waishi katika matumaini na maendeleo.Mwisho.

Post a Comment