Na Amini Nyaungo
Kuchelewa kujengwa kwa kiwango cha lami kipande korofi cha barabara kutoka Igauri, Ilongero hadi Haydom mkoani Manyara kimeendelea kumtesa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mheshimiwa Ramadhan Ighondo akiendelea kuililia Serikali na kila sehemu anapona kunaweza kuleta msaada wa kujengwa kipande hicho cha Barabara.Hayo yametokea jana (Januari 15,2025) katika kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Singida ikijadili mambo mbalimbali ya miundombinu ya Barabara.
Ighondo alipata nafasi ya kuwakumbusha wajumbe waliohudhuria pamoja na Serikali kuwa wananchi wa Jimbo lake wanayetumia barabara hiyo wamekuwa wanyonge kwa kutokukamilishwa kwa barabara hiyo ambayo tayari imepangiwa bajeti kilichobaki Wakandalasi waanze kazi ya kuijenga."Wananchi wangu wa Jimbo la Singida Kaskazini wanashauku ya kuona barabara ya lami ikipita katika ardhi yao," Ighondo.
"Wananchi wa Singida Kaskazini wanayo hamu kuona hii Barabara ya Singida- Igauri - Ilongero na Hydom inajengwa Kwa kiwango cha Lami. Zile Km 11.5 tulizoahidiwa kwenye bajeti ya 2023/2024 kwamba zitajengwa Kwa kiwango cha Lami".Aidha, Aidha kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa Wilaya, Wabunge, viongozi wa dini na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambapo Ighondo ni Makamu mwenyekiti wa Bodi hiyo.
"Mwisho.
Post a Comment