NATAKA MKALAMA IWE KAMA KIZIMKAZI- KISHOA


Na Amini Nyaungo
Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kuwa kama Kizimkazi ya Rais Samia Suluhu Hassan hili ni wazo la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Jesca Kishoa alilolitoa usiku wa kuukaribisha mwaka mpya 2025.
Hayo yamefanyika jana Nduguti  Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ambapo Mbunge wa Viti Maalam Jesca Kishoa aliwakaribisha Wananchi nyumbani kwake kwa ajili ya kusherehekea na kuukaribisha mwaka mpya wa 2025.
Katika salamu zake kwa Wananchi Kishoa amesema kuwa anatamani kuiona Wilaya ya Mkalama inatambulika zaidi na inakuwa kama Kizimkazi anakotokea Rais Samia Suluhu kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo upo ikiwa na lengo la kuitangaza Wilaya hiyo ili kupata fursa mbalimbali.
"Nataka Wilaya ya Mkalama itambulike zaidi nataka iwe kama Kizimkazi kuanzia sasa na kuendelea,"Kishoa.

Chamber Talkshow imewatafuta wananchi waliofika eneo hilo wamesema wamefurahishwa na tukio hilo ambapo Saidi Maulid amesema..
"Tumefurahi  mimi nimeona vitu ambavyo sijawahi  kuviona sehemu nyingine, vitu kama hivi tunavionaga katika Televisheni tumeipokea vizuri," Maulid

Naye Hamis Ali amesema kuwa juhudi anazozifanya Kishoa wanakubali kwa kazi nzuri anayoifanya 
"Kwa juhudi alizo nazo tunamuona anatufaa sana 2025 lazima tuupige mwingi, mtu anaye tupambania , wilaya hii tumepata mtetezi ambaye ni Jesca Kishoa,"Hamis.

Kwa upande wake Mwanchi Msolawi Bakari naye amesema kuwa ameupokea vyema mwaka 2025 na kujivunia kuwa na Kishoa Wilaya ya Mkalama.
" Tumeupokea kwa shangwe mkubwa hii ya kwangu kama ya pili kwa ukubwa  baada ya Kizimkazi, tunajivunia sana kuwa na yeye kishoa, ni mpambanaji," amesema

Kwa upande wa Farida Masengi amemshukuru Kishoa kwa uwepo wake huku akikiri kuwa amewafanyia mambo mengi sana.
" Tunampenda Kishoa ametutendea mengi makubwa , kwa sisi kina mama anatutembelea na kutuunga mkono kwa mambo mengi, tunamuombea awe mheshimiwa rasmi," Kishoa
Kishoa amewakaribisha Wananchi wa Mkalama nyumbani kwake na kuahidi kuendelea na furaha hiyo kila mwaka na kuahidi kuiweka katika ramani Wilaya ya Mkalama.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post