Na Amini Nyaungo
Wanasiasa wamekuwa na sarakasi nyingi sana yaani urafiki wao hauna maisha marefu leo marafiki kesho maadui, nani alidhani Peter Msigwa angehamia CCM ? Nani aliamini hayati Edward Lowasa angehamia CHADEMA ? Nani aliwaza Benard Membe angeihama CCM ? Hivi ulifikiria Zito Kabwe angeanzisha chama chake ?Hayo maswali ambayo najiuliza hapa na naona kabisa Tundu Lissu akianzisha chama chake cha Siasa na akaendeleza harakati zake huko za siasa na mambo yakaendelea nitakwambia kwa nini kwa mtazamo wangu.
Hebu ngoja Dokta Vicent Mashinji aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA tena yeye wa nne wa chama hicho tangu kuanzishwa alihamia CCM Mwaka 2020, David Kafulila alihamia CCM.Mwaka 1995 Chama cha NCCR Mageuzi kilikuwa na nguvu sana James Mbatia na Mrema walikuwa mafahali wawili na baadae ndoa ya urafiki wao ilikufa Mrema alianzisha chana chake na Mbatia alibakia NCCR Mageuzi.
Stori inaanzia kwa Zitto Kabwe yeye pasipo kutegemea alienda kuanzisha Chama chake cha ACT Wazalendo ambapo huenda kikawa ndio chama kikuu cha upinzani baada ya miaka kadhaa na ametia nia ya kuutaka Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kama kutakuwa na kumeguka kwa CHADEMA basi Kabwe atakuwa chama cha upinzani, chama kikuu cha upinzani ni kipi ? Ni kile ambacho kinawafuasi wengi kuliko vyama vingine vya upinzani.
Mfano CHADEMA ni Chama kikuu cha upinzani kwakuwa kina wafuasi wengi lakini hata matokeo ya uchaguzi huwa kinakuwa cha pili baada ya CCM ndio maana kimekuwa chama kikuu cha upinzani pamoja na kuwa na wawakilishi wengi zaidi kuwazidi wengine wa Upinzani.
LISSU ATAANZISHAJE CHAMA CHAKE ?
Njia ambayo aliyopitia Zitto ndio naiona kwa Lissu shida ilianza kwa Mwenyekiti wa Chama chao baada ya sintofahamu na kutoelewana akaanzisha chake.
Sauti inayotembea mitandaoni ambapo Lissu ameulizwa juu ya kinachoendelea na kunukuu baadhi ya maneno ya Mwalimu Nyerere akiyaweka kwa CHADEMA ya kuwa
"Nimekaa CHADEMA kwa miaka 20 nitabakia CHADEMA lakini CHADEMA sio Mama yangu, kama watakiuka misingi ambayo imenifanya niiingie CHADEMA nitahama,"
Kauli yake hii inatoa maswali mengi sana Lissu ni mwanasiasa ambaye anaushawishi mkubwa sana kila mmoja anaweza akasema kuwa atahamia CCM au ataenda ACT Wazalendo akutane na Zitto lakini huku kwa Kabwe misimamo aliyonayo na dira ya Lissu unaona kabisa hawaendani japo kama unabeti basi huku weka "GG" yaani kuna uwezekano.
Juu ya kuhamia CCM itakuwa kazi ngumu kidogo kwake japo nao CCM wanahitaji turufu kama aina hiyo ya Lisu ili wamalize shughuli mapema je ataenda wapi ?
Ndipo ambapo naona akaanzisha chama chake na hatimaye kuunda upya na safu yake ili kije kupambana na vyama vilivyopo hivi sasa.
Ndani ya ubongo wake anaona kabisa anauwezo wa kuwa na watu nyyma yake wtaakaomsaidia kuanzisha chama chake na kikadunda kama ambavyo Zito alivyoweza kukiweka ACT katika ramani.
Hii kauli yake imenifanya niwaze mengi mno lakini majibu ya maswali yangu yapo karibu mno.
Mwisho.
Post a Comment