Na Jumbe Ismailly
DARAJA HILI SIO MIONGONI MWA MADARAJA YALIYOTENGENEZWA MKALAMA
WAKALA wa barabara Mjini na vijijini (TARURA) wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida imetumia shilingi 726,596,220/= kukamilisha ujenzi wa barabara ya Gangerankuru Moma kwa kiwango cha lami pamoja na matengenezo ya muda maalumu barabara ya Iguguno Lyelembo-Msingi na ujenzi wa madaraja mawili ya mawe.
Meneja wa Tarura wilaya ya Mkalama,Eng.Rahabu Thomasi amefafanua kwamba kati ya kiasi hicho cha fedha,shilingi 502,474,000/=kilitumika kukamilisha ujenzi wa barabara ya Gangerankuru Moma yenye urefu wa kilomita 0.64.
Aidha Eng.Rahabu ameweka bayana pia kwamba shilingi 224,122,220/- zimetumika kwenye matengenezo ya muda maalumu ya barabara ya Iguguno-Lyelembo-Msingi yenye urefu wa kilomita 4.33 na ujenzi wa madaraja mawili ya mawe kwenye barabara Igugumo-Lyelembo –Msingi.
Kwa mujibu wa meneja huyo wa Tarura mradi wa ujenzi wa barabara ya Gengerankuru Moma umeanza kutekelezwa sept,20,mwaka 2023 na kukamilika mei,16,mwaka 2024 na kuzitaja kazi zilizofanyika kuwa ni pamoja na ujenzi wa kitanda cha barabara,uwekaji wa tabaka la kwanza la udongo G25,uwekaji wa tabaka la pili la udongo G25,uwekaji wa tabaka la juu la lami lenye urefu wa kilomita 0.64,ufungaji wa taa kumi za barabarani na ujenzi wa mifereji.
Hata hivyo Eng Rahabu amesema ujenzi wa barabara hiyo umegharamiwa na serikali kuu kupitia fedha za tozo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 ambapo shilingi 502,474,000/= zimetumika.
Faida za mradi huo kwa wananchi wa Kijiji cha Nduguti ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri kwa wananchi kufika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya.
Akifafanua kuhusu mradi wa uliopo katika vijiji vya Kidi na Yulansoni, uliotengenezwa na Mkandarasi M/S TIMAJO ENGINEERING COMPANY LTD wa Makambako,Eng.Rahabu amesisitiza kwamba ulianza kutekelezwa sept,20,mwaka 2023 na kukamilika machi,18,mwaka 2024 na kuzitaja kazi zilizofanyika kuwa ni pamoja na kuinua tuta la barabara,kuweka changarawe kwenye sehemu korofi na kujenga madaraja mawili ya mawe.
MWISHO.

Post a Comment