VIJANA NYIE NGUZO YA TAIFA-WILIAM NYALANDU

 Na Amini Nyaungo

Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kusimama imara kuilinda na kutunza Tanzania kwa nguvu ari pamoja na moyo ili urithi ulioachwa na waasisi wa Taifa uendeee kudumu.

Hayo ameyasema leo tarehe 16.12.2024 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Vijijini ndugu William  Nyalandu alipokuwa anaongea na Umoja wa Vijana wa Chama hicho ilongero Mkoani hapa.
Nyalandu amesema vijana wanatakiwa wajitambue na kuwa wazalendo kwa taifa lao kwani vijana ndio nguzo ya uongozi wa miaka ijayo.

"Vijana nyie ndio nguzo ya taifa , taifa linawategemea kuweni wazalendo," Nyalandu


Aidha ametumia fursa hiyo kuwaambia kuwa CCM imebahatika kumpata Rais Samia Suluhu Hassan katika kuongoza nchi ya Tanzania.

"Tumebahatika kupata Rais mwenye maono makubwa sana kwa taifa hili, sio tu kiongozi bali ni kiongozi mwenye maono ya kuendesha taifa mbele,"Nyalandu

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post