Na Amini Nyaungo
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Singida Vijijini umetoa tamko kali kwa viongozi mbalimbali kuanza kufanya kampeni ambazo hazina tija ndani ya chama hicho.
Hayo ameyaongea leo tarehe 16,12,2024 Ofisi ya Chama hicho Ilongero mkoani Singida walipokuwa katika Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali ya chama hicho.
Thabiti ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya viongozi wanatoka mahali mbalimbali wanaenda kuharibu siasa katika Wilaya ya Singida Vijijini na kuwaambia kuwa waache mara moja wakiendelea kufanya hivyo watajua namna gani watafanya kukomesha hayo yanayoendelea."Umoja wa Vijana Singida vijijini hatutaki siasa chafu , hatutaki watu waje wafanye siasa zisizo na maana,kuna watu wanatoka sehemu mbalimbali kuja kuharibu kwetu hatutaki na wakiendelea tutajua kipi cha kufanya kama Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi," Thabiti.
Katika Baraza hilo lilihudhuliwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini William Nyalandu akiwaomba vijana kutulia na kuwa wazalendo ili walilinde taifa."Nyie vijana ndio msingi wa taifa letu hivyo tunawahitaji sana mlilinde taifa," Nyalandu
Post a Comment