Waandishi wa Habari wa mikoa ya Singida na Simiyu wamepatiwa mafunzo ya kujitambua na kujiweka sawa katika taarifa wanazozitoa kwa jamii.
Mafunzo haya yametolewa na Wadau wa 'Kijani Hai' Helvetas na GIZ kwa pamoja wamewapatia mafunzo hayo wanahabari kutoka Radio na Maafisa Habari wa Wilaya kutoka mkoa wa Singida na Simiyu kuanzia Desemba 10 hadi 12,2024 yaliyofanyika Manyoni Mkoani Singida.
Mara baada ya mafunzo hayo Emmanuel Lufilisha ambaye ni Afisa wa Uhifadhi na Bioanuai katika Mradi wa Kijani Hai amesema kuwa wamewaleta waandishi wa habari ili wapate ujuzi zaidi na waendelee kuandika mambo mbalimbali mazuri ya taifa.
Aidha Lufilisha amesema ndani ya mafunzo hayo pia wamewaelezea umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na kukijanisha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kulinda rangi ya kijani.Lufilisha amesema kuwa mradi wao unahusisha mikoa ya Simiyu na Singida ambapo mradi huo unalinda mazingira pamoja na kilimo hai.
" Mradi wetu unahusisha mikao miwili ya Simiyu pamoja na Singida , mradi wetu unalinda mazingira pamoja na kilimo hai,"Lufilisha.
Katika hatua nyingine mafunzo hayo yalisimamiwa na Maiko Onesmo pamoja na Lilian Urio ambao kwa pamoja walitoa mafunzo mbalimbali ikiwemo matumizi ya Teknolojia kwa Wanahabari, Kuongeza ujuzi kuendana na wakati wa sasa, Kujiamini pamoja na kutafuta fursa mbalimbali zinazopatikana.
Kwa upande wake Lilian Urio ambaye ni Mshauri wa Maswala ya Mawasiliano na Mzalishaji Maudhui amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanahabari pamoja na kuwapa nyenzo za kufanyakazi zao ziwe rahisi pamoja na kuendana na mazingira.
"Tumewapa mafunzo wanahabari ili wafanyekazi zao vizuri pamoja na kuwaanda kwendana na Teknolojia," UrioKwa upande wa Maiko Onesmo yeye amewaasa wanahabari kuwa wabunifu na kujiamini ili waweze kufanikiwa katika kazi zao kujiamini kwao na ubunifu kutawafanya waaminike na kufanikiwa kwa wanachokitaka.
Kwa upande wa wanufaika ambao ni wanahabari wamewashukuru Helvetas kwa kuwaletea wawezeshaji ambao wamewapa kitu kipya katika kufanikisha kazi zao.
Johnson Edward Mtangazaji kutoka Standard Radio amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka wakati huu ambao Teknolojia imehama hivyo wataendelea kuyafanyia kazi waliyoyasoma." Naamini hii imekuja wakati muafaka teknolojia imebadilika na sisi tutaendana na mfumo huo," Johnson
Mwakilishi TBC kutoka mkoani Singida Jamaldin Abou amesema kuwa swala la ubunifu pamoja na kujiamini walilolitoa Wawezeshaji litamfanya kuongeza ujuzi na maarifa zaidi katika kazi zao."Mimi sijaja bure nimepata vitu vingi vya msingi, kujiamini na ubunifu hasa kazi zetu zinahitaji sana ubunifu," Jamaldin
Huku Mwanahabari kutoka Bariadi Alex amewapongeza sana wawezeshaji kwa kutawala mafunzo kwani walichokiwa wanakifundisha kina maana na msingi mkubwa katika kazi zao za kila siku.
Rangi ya kijani inapendeza sana ipo katika bendera yetu ya taifa la Tanzania ukiangalia vyema utaiona upande wa juu wa bendera, hivi ndivyo ambavyo jamii na wanaharakati wanajaribu kuiweka nchi katika rangi ya kijani kama wafanyavyo Helvatas.Mwisho.






Post a Comment