Leo ni maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo mkoa wa Singida iliadhimisha kwa kupanda miti katika Hospitali ya mkoa wa Singida na sehemu mbalimbali.
Viongozi mbalimbali walikuwepo akiwemo Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata , Godwin Gondwe Mkuu wa Wilaya ya Singida na viongozi wengine pamoja na Wananchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata akiwa katika zoezi la upandaji miti katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe akiwa katika zoezi hilo la upandaji miti katika kusherehekea Uhuru miaka 63.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Singida wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Martha Kayaga naye alikuwepo katika upandaji wa mitiPhoto Credit: SNADA REAL ONLINE TV









Post a Comment