UKITOKA NYUMBANI MUAGE JIRANI YAKO- MUNGWANA

 Na Amini Nyaungo

Kuelekea kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya Kamishana Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Singida Hamisi Mungwana ameiasa Jamiii kuwaaga jirani zao wanapotoka nyumbani ili kupekuka wizi na udokozi majumbani.
Ameyasema hayo leo tarehe 18.12.2024 katika Standard Radio kipindi cha asubuhi cha Zinduka akitoa elimu juu ya usalama wa Raia na mali zao.

Mungwana amesema ni vyema kuwe na mawasiliano mazuri pale unapotka nyumbani itasaidia hata jirani yako kujua kuwa haupo kama ikitokea lolote ataweza kusaidia.
"Niwaombe majirani muwe na mawasiliano mazuri ili kuondoa udokozi na wizi unaotokea majumbani," Mungwana


Katika hatua nyingine Mungwana amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa wawe makini katika usafiri wachague magari mazuri ambayo yanaweza kuwafikisha salama wanapoenda huku akiwaomba madereva wasio rasmi wasijihusishe na udereva.
"Natoa wito wale wasafiri wasisafiri kwa magari ambayo yanashaka nayo na wale wote madereva ambao huenda wamechoka kutoka safari ya mbali basi wapunzike inapofika mahali wameshindwa kuongoza safari," Mungwana.
Katika mazungunzo yake Mungwana amewaomba wananchi kuunda Ulinzi shirikishi kwani katika maeneo yao ili kuimarisha hali ya usalama, amesema kuwa maeneo ambayo yana ulinzi shirikishi yanausalama zaidi kuliko yale ambayo bado hawajaunda vikundi hivyo.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post