SIRI YA USHINDI CCM WILAYA YA IKUNGI YAFICHUKA
Amini Nyaungo
0
Na Amini Nyaungo
Kazi nzuri na maneno yanayojenga ndio sababu ya ushindi iliyoupata Chama cha Mapinduzi (CCM) Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Joshua Mbwana Hungura alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) zilizopo wilayani hapa.
Hungura amesema kuwa CCM imefanikisha miradi mingi ya maendelo ndani ya Wilaya hiyo ikiwemo Shule, Barabara pamoja na Umeme hivyo wananchi wapo makini na kuona namna gani chama hicho kinafanyakazi yake vizuri.
Aidha katika hatua nyingine Hungura amesema kuwa matokeo hayo ya uchaguzi wa serikali za Mitaa ndio ambavyo itakuwa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Post a Comment