Na Amini Nyaungo
Baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa zilizofanyika Novemba 27,2024 kutamatika sasa muda wa waliochaguliwa kuanza kufanyakazi mara moja katika hali ya haki, busara na Weledi.Ndivyo ambavyo Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Singida na Diwani wa kata ya Majengo Yagi Maulid Kiaratu alivyowaasa Wenyeviti hao waende kufanyakazi kwa bidii na isiyokuwa na migogoro.
Hayo ameyasema jana Desemba 3,2024 wakati alipowaita Wenyeviti waliochaguliwa kwa ajili ya kuwapa mihuri ya kufanyiakazi zao za kila.Kiaratu amesema kuwa Kata ya Majengo wanahitaji maendeleo zaidi hivyo wamepewa dhamana hiyo nawao waitumie vizuri katika eneo lao.
"Kata ya Majengo tuna namna yetu ya utendaji kazi, tunataka maendeleo zaidi pamoja na mshikamano ili tufanye vizuri zaidi katika kata yetu,"Kiaratu
Pia amewaomba wasiitumie mihuri vibaya kwa wananchi wao wanaowaongoza katika moja ya maagizo yao wakati wanaomba kura ilikuwa juu ya hiyo mihuri endapo mwananchi akitaka huduma wengine hulipishwa.Mstahiki Meya jana aliwaita wote waliochaguliwa nafasi ya Wenyeviti wa kata ya Majengo na kuweza kuwapatia mihuri kwa pamoja.
Mwisho

Post a Comment