Na Amini Nyaungo
Waandishi wa Vitabu wametakiwa kuandika ujumbe sahihi unaoakisi jamii ya Tanzania na tamaduni zao ili dunia ijue thamani ya nchi hii na mambo mazuri yalipo ndani yake.
Hayo ameyasema leo tarehe 06.12.2024 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Rehema Sombi alipoongea na Standard Radio juu ya uzinduzi wa kitabu chenye historia ya Mkoa wa Singida ambacho kinazinduliwa siku ya kesho mkoani hapa mgeni rasmi atakuwa ni Profesa Palamagamba Kabudi Waziri wa Sheria na Katiba.
Aidha Sombi amesema kitabu hicho kitailezea Singida pamoja na historia zake vizazi na vizazi wataisoma na kuelewa vilivyomo mkoa wa Singida pamoja na vivutio vyake.
"Kuiandika historia ya Singida ni kuweka urithi wa taifa na mkoa mzima, hii itabakia milele na milele katika mkoa huu , vizazi na vizazi watakuja kusoma na kuijua Singida kiundani,"Sombi
Sombi amewaomba watu wote kufika katika uzinduzi huo ambao utafinyika siku ya kesho tarehe 07.12 2024 katika ukumbi wa Aqua Hoteli
Kitabu hiko cha Historia ya Singida kimetungwa na Alfredi Ringi kijana mzaliwa wa mkoa wa Singida maeneo ya Misimko Wilaya ya Singida Vijijini.Mwisho.
Post a Comment