GWAU AMUUNGA MKONO SAMIA NISHATI SAFI, KIDEKA WACHEKELEA

 Na Amini Nyaungo

MBUNGE wa  Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau  ametoa mitungi 60 ya Gesi kwa wakina mama wa kata za Ilongero, Kijota na Mtinko ikiwa na lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Hayo ameyafanya leo Desemba,21,2024 katika kata za Ilongero, Kijota na Mtinko akisema kuwa ameleta gesi hizo ili kuwasaidia kina mama watumie nishati safi ya kupikia  kama ambavyo Rais Dokta Samia Suluhu Hassan  anavyohimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
"Rais Samia amelipa kipaumbele sana matumizi ya gesi mbadala ya kupikia, anatamani kila mmoja awezekutumia nishati hii ndio maana na sisi wasaidizi wake tunaendelea kumuunga mkono ndio maana leo natoa mitungi ya gesi,"Gwau
Gwau ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu akitaka amani hiyo iendelee katika maisha yao yote kama ambayo  waasisi wa taifa hili walivyo acha amani na utulivu.
"Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kufanya uchaguzi kwa amani pamoja na  hayo basi tuilinde amani yetu iliyopo hapa nchini kama tulivyoachiwa urithi na waasisi wa taifa hili," Gwau
Aidha amewashukuru viongozi mbalimbali ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ndani ya jimbo hilo pamoja na madiwani wote wakimewo wa viti maalumu.


Kwa upande wa kina mama ambao wamenufaika na mitungi hiyo ya gesi wamefurahishwa kwa kupatiwa nishati hiyo na kuahidi kuanza kuacha matumizi ya nishati chafu ya kupikia.
Alfonsina Jonas amesema kuwa ataendelea kutumia gesi hata inapoisha atajaza tena ili na yeye kumuunga mkono Mbunge wa viti maalum pamoja na Rais Samia anavyohimiza.
"Mimi nitaendeleza kutumia gesi hii hata pale itakapoisha nitajaza tena ili nifuate vile Rais Samia anahimiza pamoja na Mbunge wetu wa Viti Maalum Martha Gwau," Alfonsina
Naye Nuru Ramadhani amesema kuwa gesi aliyoipata leo itamsaidia katika matumizi yake ya kila siku na kumshukuru Martha Gwau kwa kuwajali kwa kuleta gesi.

Aidha Gwau baada ya Ilongero akatoa mitungi ya Gesi kijiji cha Kideka kilichipo Puma kwa wafanyabiashara  pamoja na kofia kwa ajili ya kujikinga na jua pa.oja na pochi za kuwekea pesa zao.


Wakati anatoa Gesi Kideka Mhe. Martha Gwau amepongeza juhudi hizo za Serikali na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.
Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuasisi mpango huo wa nishati safi kwa wanachi huku akitoa ruzuku kwa wananchi kwa ajili ya kwenda sambamba na mpango huo wa serikali.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Bw Mika Likapakapa amesema kuwa mradi huo unaimarisha matakwa na utekelezaji wa ilani ya CCM kama ambavyo imeainisha kuimarisha sekta ya nishati kuwa na nishati safi ya kupikia sambamba na kuhifadhi mazingira ya Tanzania.
MWENYEKITI WA CCM WILAYA IKUNGI AKIKABIDHI MITUNGI YA GESI BAADA YA KUUNGANA NA MBUNGE MARTHA GWAU



Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post