Na Amini Nyaungo
Jamii imetakiwa kuwa waminifu katika ndoa zao ili kupunguza migogoro pamoja na magonjwa mbalimbali yakiwemo mamambukizi ya virusi vya Ukimwi.Hayo ameyasema leo tarehe 01.12.2024 Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Godwin Gondwe ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singia Halima Dendego alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambapo kwa mkoa wa Singida yamefanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania.
Gondwe amewahimiza wakazi wa Singida na Tanzania kuwa waaminifu katika mahusiano ili kuepusha mambo mengi ya magonjwa kwani kufanya hivyo kunaweza kuepusha ugomvi katika ndoa pamoja na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
"Niwaambie mnatakiwa muwe waaminifu katika ndoa na wote walio kukaribia kuoa, hii itaepusha vitu vingi ikiwemo migogoro ya ndoa pamoja na magonjwa," GondwePia Gondwe amewaomba wanafunzi kuacha tamaa ya vitu vidogo vidogo ambavyo vinapelekea wanaingia katika mahusiano yasiyosalama na kushababisha kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Katika hatua nyingine ameiasa jamii kuwapenda na kuwajali wale ambao wamepata Virusi vya Ukimwi wasiwatenge.
"Tushirikiane nao wanaoishi na virusi vya Ukimwi tusiwatenge,"Gondwe.
Aidha katila maadhimisho hayo wadau mbalimbali walikuwepo kuhakikisha maadhimisho hayo yanaenda vizuri, USAID Afya Yangu kwa mkoanwa Singida akiwakilishwa na Mkurugenzi wao Saidi Mgeleka amesema kuwa wao wanahakikisha kila kitu kinaenda vizuri katika kutoa ushauri na kuwasaidia waathirika.
"Sisi tunaendelea na kupambana ili tuondoe maambukizi kwa kutoa elimu ya kujikinga pamoja na kuwapa ushauri wale ambao tayari wamepata maambukizi ya virusi vya Ukimwi," Mgeleka
Kwa taarifa iliyopo maambuzi ya virusi vya Ukimwi kwa watu waliofikiwa ni elfu 27632.
Kauli mbiu ya mwaka huu wa 2024 juu ya Maadhimisho ya virusi vya Ukimwi ni ''Chagua njia sahiji tokomeza Ukimwi"
Mwisho



Post a Comment