KIKOSI CHA MLATA SINGIDA, YAGI, IGHONDO, KINGU, KISHOA NDANI

 

Na Amini Nyaungo
Martha Mlata Mbunge wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Muimbaji wa Nyimbo za Injili pamoja na mwanasiasa mbobevu ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida.

Kwa hakika mama yetu huyu anaendesha vyema sana Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida hasa kwa kuonesha tabasamu muda wote ila ukienda kinyume utajua yeye nani lakini ni mtu makini sana katika uongozi.
Chamber Media leo tumeona tumpangie kikosi chake ambacho anakiongoza Mkoani Singida kuipeperushaa bendera ya CCM ikiwa   moja ya mikoa iliyochangamka sana kisiasa.

Mlata ndio bosi wa viongozi wote wa mkoa huu kwa chama chake cha Mapinduzi kwahiyo yeye atakuwa kocha huku safu yake ya mashambulizi itakuwa na wachezaji mchanganyiko.

Kabla ya yote tujue kwanza mkoa huu wa Singida sehemu zake maarufu ambazo ni Iramba, Manyoni, Singida Mjini, Singida Vijijini, Mkalama, Ikungi na Itigi.

Kilosi chenyewe hiki hapa kitakachocheza na mikoa mingine mtaamua kicheze na mkoa upi ?

1. Ramadhani Ighondo
Huyu ni Mbunge wa Singida Kaskazini jimbo hili amelitendea haki kwa kiasi kikubwa kazi iliyofanyika kubwa sana, Ighondo anachukua nafasi ya ulinzi wa goli kipa akiingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Mlata mkoani Singida.
Ighondo anaongea sana na simu kwa watu wake jimboni kwake muda wowote ule utakao mtafuta ni mtu na nusu anajua sana kujipozisheni na kujitengea nafasi ili afunge ndio maana jimbo lake liko vyema sana kula tano Ighondo.


2. Elibariki Kingu
Huyu jamaa mjanja sana,mwanaharakati sana yaani namfananisha na Diamond Platnumz anajua sana kujipenyeza ni Mbunge wa Bunge la dunia akifanya vyema sana.
Sijawahi kufanya nae kazi ila kazi zake naziona, ujanja aliobarikiwa pamoja na kupiga kazi usiku na mchana na yeye kaingia katika kikosi cha Mlata kinachoiwakilisha Singida kucheza na mikoa mingine ya Tanzania mitano tena Kingu.
Kingu yeye hasubiri afanyiwe anaenda chaka kwa chaka kuwafuata wananchi kuangalia nini hakijakaa sawa anarekebisha.

Huenda asitumie nguvu sana mwakani kama nia na lengo likiwepo maana kila kitu amefanya katika Jimbo lake, hii ni turufu ya mkoa wa Singida.

Kingu yupo jimbo la  Singida Magharib msijisahaulishe.

3. Yagi Kiaratu 
Huyu ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida bila shaka kazi anayoifanya ni kubwa sana kuunganisha watu pamoja na kuzuia mashambulizi.
Katika maisha ya kawaida mama yetu huyu anatoa sana japo hataki kujionyesha, hatoi ili aonekane bali anatoa kwa imani na jofu ya Mungu anafanyakazi usiku na mchana.


Anaongoza vizuri sana, sio tu maswala ya siasa bali hata kwenye futiboli yupo yeye ndio anayeongoza soka la wanawake na ndio anayedhamini ligi ya wanawake Singida.

Yagi anafanya vizuri sana anajua kumsoma mtu yoyote kisaikolojia.


Yagi mitano tena ni mtu na nusu sana na anafaa kuvuka kiunzi hapo alipo apande zaidi atasaidia sana wananchi wa Singida pamoja na kuimarisha safu ya wachezaji wa Mlata.


4. Mohamed Msaghaa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Singida Mjini, wengi wanaeza wakajiuliza dogo huyu kaingiaje, sisi ndio tunakaa naye.
Anajua sana kuwaunganisha vijana, kama CCM itashinda katika chaguzi mbalimbali za Singida Mjini huyu dogo anamchango mkubwa sana ni kijana wa kuchungwa sana maana naamini miaka ijayo huenda akapenya zaidi na zaidi na kuwa sehemu ya juu kwa harakati zake.

Siasa anaijua na anaendelea kupambana ili wanachama wengi zaidi waingie ndani ya chama.

5. Amisa  Msele
Huyu dada mdogo kabisa ni Mjumbe wa Baraza kuu Umoja wa Vijana wa Chama Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa akitokea Mkoani Singida.
Huyu ukimchana katika ngozi yake anatokea CCM anapenda sana chama sijui maisha yake ya kwao akiwa na mapenzi haya ya CCM basi familia yake itakuwa inafaidi sana namna anavyoishi na CCM yake.

Lakini sio hivyo tu anajua sana kuongea anajua sana kuweka hoja zake popote anapoenda kuongea. Nadra sana vijana kama hawa kuwapata na wameingia katika kikosi cha Mlata yeye na Msaghaa hongereni chapeni kazi.

6. Mwigulu Nchemba
Mbunge wa Iramba Magharibi huyu ndio nahodha wa kikosi hiki akiwaongoza wabunge wote akivaa usinga wa unahodha, ni Waziri wa Fedha lakini pia ni mtu wa watu Iramba wanamuelewa sana kwa jitihada zake kuwaletea maendeleo.
Wale waliosema Iramba Nkulu kuliko Tanzania ukimuuliza Nchemba ataweza kuwa na jibu sahihi anajitahidi sana, huyu bwana siasa anazijua sana kama muimbaji basi Ali Kiba ukisema wanamuziki wanaojua kuimba pamoja na mashairi mazuri basi ni Mwigulu Nchemba.
Hongera sana kaka najua hakuna namna kazi ipo mwakani kilichobaki wewe umalize tu mambo madogo ila kazi kubwa ushaifanya jimboni kwako.

7. Miraji Mtaturu
Anashikilia Jimbo la Singida Mashariki amepata nafasi ka kusukuma maendelea katika jimbo lake shule na miradi mbalimbali ikifanyika.

8. Jesca Kishoa
Huyu ni Mbunge wa viti Maalumu ukienda Mkalama ukiuliza nani unamjua huku basi watakuambia Kishoa mitano tena, ni mdada ambaye anajua sera anajua kucheza na muda unaweza ukashangaa kaingiaje hapa sisi tunamuandika yoyote anayewezakazi na kuleta maendeleo Kishoa kala dimba la kati anapambana sana ili Mkalama na Singida ing'are.

Anatendea haki sana Ubunge wake kwa kuwatumikia wananchi wake
Naamini kama anvyofikiria basi Mkalama itakuwa Mkalama miaka ijayo, sitaki kuhojiwa jinsi navyofikiria ila naiona Mkalama mpya.

9. Baraka Hamisi\Mohamedi Omari 
Hapa mmoja ataanza nani wakumpisha mwenzake wataelewana wenyewe, Baraka ni diwani wa kata ya Mandewa kama Wilaya vile ina watu elfu 42,000 naamini huko mbele itapinguzwa kijana huyu anajitahidi sana kuleta maendeleo pamoja na ubunifu alionao.
Mohamed Omary huyu yupo Ipembe , ukizungunzia kata ya Ipembe unaongelea Singida, Soko kuu la Singida lipo kwake hapendagi kujionyesha ila maendeleo yanaongea.

Utashangaa kwanini hawa Madiwani wamekaa nafasi ya ushambuliaji ? Hawa ndio wenye Singida yao lazima wakae waweke magoli.
Hongereni sana madiwano wawilo walioingia katika kikosi cha Mlata.

10. Mussa Sima
Mbunge wa Singida Mjini anafanyakazi vizuri sana analeta maendeleo kaingia katika kikosi hiki cha Malata.

11. Martha Gwau
Ni Mbunge wa viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi anafanyakazi nzuri anaendelea kukipeperusha Chama kwa namna awezavyo ameingia katika kikosi hiki na kufanya mashambulizi ya maendeleo.
Jamani wapo wengi sana ila hawawezi kuingia wote katika kikosi kikubwa kazi ziendelee.

TUUJUE KIDOGO MKOA WA SINGIDA
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania mkoa huu upo kanda ya kati ukipakana na mikoa ya Manyara upande wa Kaskazin, Upande wa Mashariki unapakana na Dodoma, Magharib unapakana na Tabora Shinyanga na Msimbo wa Posta ni 43000
Katika Sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 2,008,058 kutoka watu 1,370,637wa mwaka 2012

Wakazi wa wilaya za Singida mjini pamoja na Wilaya ya Ikungi Wanyaturu ambao nao wamegawanyika katika makundi matatu Warirwana, Wahi na Wanyamnying'anyi , huku Wilaya ya Iramba Walio  ni Wanyiramba  na wakiwa Wagogo  wengi huko Manyoni  pia kati ya wenyeji kuna Wanyisanzu,  na makabila mengine madogo.

Mazao kama vile Alizeti ambalo linaitambulisha Singida, Vitunguu, Mtama, Mahindi, Wele ni mazao ambayo yanastahi mkoani Singida.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post