UTOFAUTI WA WANYATURU NA WANYIRAMBA

Na Amini Nyaungo

Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa ambayo inavitu vingi vyenye kuvutia moja wapo aina ya watu waliopo Wanyaturu pamoja na Wanyiramba, hawa ni watani wa jadi makabila mawili makubwa kuna kabila moja Wanyisanzu ila hili dogo sana halina watu wengi.
WANYATURU WAKICHEZA NGOMA ZAO ZA ASILI

Wanyaturu wanapatikana zaidi Ikungi na Singida Mjini hawa wana utofauti na wale wa Iramba ambao wengi wao ni Wanyiramba, unaweza kuwatofautisha vipi leo nakupa walivyo.

WANYATURU
Wanyaturu weupe sana kwa wanawake wana maumbo mazuri yale yaliyoimbwa kuwa namba nane na "Daz Baba", warefu sura zao nyembamba mithili ya Wahabeshi.

Wanavutia sana kuwaangalia, ''Nyashi" sio kubwa sana ila umbo limechorwa ukitaka nyashi nenda Iramba ambapo nitakujakukueleza chini.
Sifa yao nyingine hawa Wanyaturu wamegawanyika mara mara tatu  yaani Wahi, Wairwana na Wanyamnying'anyi
walio Singida mjini kuelekea Ikungi na wale wa Wairwana ambao watata sana hawa wakutoka Ilongero yaani kidogo wagomvi kukimamsha hawachelewi.

Lakini hawa wa Ikungi sio watata wapole na weupe sana vijana wa Dar es Salaam wakifika huku hawarudi vizuri kwa kuwashangaa uzuri wao.

Wanawake wa Kinyaturu wavumilivu sana katika swala la maisha kama mwanaume hayupo vizuri wanaweza kuvumilia.

Kwa wanaume nao pia weupe na warefu pia walio wengi hasa huku Ikungi,  tabia za  wanaume wa Kinyaturu wavivu kazi kubwa wanafanya kina mama (ila leo watanipiga hawa hahahaha).

Kwa mujibu wa Ramadhani Ikumbi kutokea Ikungi amesema tabia ya wanaume wa Kinyaturu kuwaachia wake zao majukumu kwa walio wengi.

"Sisi tuna tabia naona kama uvivu maana ikifika wakati tunawaachia wake zetu majukumu ndio maana unakuta wanajihusisha na biashara huko barabarani,"Ikumbi

Naye Hussein Muna kutoka Ilongero anasema tabia yao kubwa inapofika umri wa makamo wanaume wengi hawajishughulishi na kazi  wana wake zao ndio wanajishghulisha.

"Kuna wakati naona kama tunakosea ndugu  Mwandishi inafika mahali tunaacha wanawakenzetu wakatafute," Muna

Tabia zao wote kwa ujumla katika ndoa asilimia kubwa wale waliopata watoto watatu au wawili hawapo kwenye ndoa wameachana sababu hii nitakuja na makala yake nzuri nishaifanyia uchunguzi na kuwahoji wahusika hii tuiache.

Tabia nyingine ya Wanyaturu wakarimu sana katika swala zima la huruma na upendo mengine ya kawaida ambayo kila sehemu yanafanyika.
Kitu ambacho huwa watu wa Dar es Salaam tunadanganyana juu ya tabia ya mahusiano ya Wanyaturu ya kusema kuwa "Malaya" hapana hawako hivyo "Umalaya" ni hulka ya mtu yoyote yule hawakohivyo kama watu wanavyowawazia mie nina miaka minne sasa hivi sijaona hilo jambo , njooni muoe Singida mpate watoto wazuri, nitaongeza mke wa pili Singida tena navyopenda watoto weupe.

WANYIRAMBA
Hawa wapo sana katika maeneo ya Wilaya ya Iramba, warefu sio weupe sana maji yakunde.
Wanyiramba huwa wanamiili pamoja na umbo zuri yaani "Msambwanda" wa maana sana hawa kwa mujibu wa rafiki yangu mmoja jina nalihifadhi huwa anasema watata sana hata kwa waume zao kukiamsha hawachelewi.

Yaani kurudi kwa wazazi kwake sio shida ukizingua anazingua, swala la wivu liko nje nje ukibisha waliokuwa nao wanajua.

Tabia nyingine uvumilivu wanao sana yaani ni watu ambao ukifika hutotaka kuondoka kama Wnayaturu tu huu mkoa kwa ukarimu wamebadiliwa.
Wanamifugo kama walivyo Wanyaturu lugha yao huwa inavutia kusikia masikioni wakati wakiongea.

Zingatia "Msambwanda" hapo ndio penyewe kwa ujumla wake wanapendeza sana, pia wapambanaji wanawake kwa waume.

Wanyiramba pia wapo Mkalama wamejaa tele, Iguguno wamechanganyika na Wanyaturu ila walio wengi Wnayeramba.
Unaweza ukahoji mbona Itigi na Manyoni sijaigusa ? Haya maeneo walio wengi wamechanganyika wapo Wagogo kwa mfano ukienda Nkoko kule Manyoni waliowengi Wagogo na Wasukuma.

Singida imetawala amani na upendo, hakuna wizi kama wa Dar es salaam unatembea uanchati wala sio shida.

Singida inaongozwa na Halima Dendego Mkuu wa Mkoa akisaidiwa na Wakuu wa Wilaya.

Mwisho






Post a Comment

Previous Post Next Post