PAUL KAMTWANGWA TYSON KWA ALAMA

 Pambano la raundi nane kati ya Mike Tyson dhidi ya Jake Paul limemalizika kwa ushindi wa alama kwa Paul.

Jake Paul ameshinda kwa "Point" pambano lake alilocheza leo tarehe 16.11.2024 kuanzia majira ya saa mbili na dakika 20 asuhubi kwa saa za kwetu Tanzania dhidi ya Mike Tyson.

Pambano lilikuwa la raundi 8 kila raundi ilikuwa na dakika mbili.


Babu Mike Tyson amesimama kwa dakika zote licha ya miaka yake 59 wakati Jake Paul yeye ana miaka 27.


Katika mazungunzo yake Paul amesema Tyson ni legend amekua akimuona hivyo amefurahi kupambana na yeye.


Wakati Tyson akitanabaisha kuwa Jake Paul ni bondia mzuri japo alikuwa anajibu kwa ufupi sana.

Maoni yangu baada ya kuangalia lile pambano

Binafsi nilitegemea Jake angeshinda kutokana na umri wa Tyson ila kilichonishangaza babu Mike Tyson amesimama dakika zote 16 licha ya kupoteza kwa alama.

Fikra yangu nikajua angeangushwa tu ila babu tizi anafanya na kama angekuwa na miaka angalau 45 hivi nguvu zingekuwa Jakee Paul asingeshinda.

Post a Comment

Previous Post Next Post