Na Amini Nyaungo
Nyota wa Mashujaa FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Chrispin Ngushi ndiye mfungaji wa goli la kwanza ligi kuu Tanzania Bara iliyoanza kutimua vumbi Agusti 16,2024 ambapo yeye amefungo goli hilo tarehe 17.08.2024 Mashujaa walipowafunga Dodoma Jiji 1-0, katika uwanja wao wa nyumbani wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Ngushi alifunga goli la kufungua pazia la msimu dakika ya 35 yamchezo huo na kuandika historia ya kufunga goli la kwanza la mashindano hayo ambapo bingwa mtetezi klabu ya Yanga yenye maskani yake Twiga na Jangwani pale Kariakoo Dar es Salaam.
Ngushi aliwahi kucheza Mbeya kwanza kwa mafanikio makubwa kwa kufunga magoli na kuisaidia timu yake.
Baadae akapata nafasi ya kucheza Yanga ambapo hakupata nafasi akatolewz kwa mkopo Coastal Union na msimu huu anautwanga mashujaa
Mchezo wa ufunguzi Tanzania Prison dhidi ya Pamba uliopigwa tarehe 16. 08.2024 ulitoka sare ya bila kufungana.
Katika hatua nyingine raundi ya kwanza yamefungwa magoli 14 mchezo ambao umetoa magoli mengi ni ule wa Ken Gold dhidi ya Singida Black Stars ambao umetoa magoli 4, Singida wakiondoka na ushindi wa magoli 3-1 ugenini.
Katika magoli 14 , magoli saba (7) yamefungwa kipindi cha kwanza huku (7) mengine yamefungwa kipindi cha pili.
Ligi hiyo kwa sasa ipo raundi ya 11 na kupitia Chamber Media tutakuandalia magoli yote yaliyofungwa katika raundi zote.
Mwisho
No comments: