Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Singida Mjini Mohamed Msaghaa amewataka vijana kushiriki mambo mbalimbali ya Kijamii ili kutengeneza mahusiano mazuri na jamii.
Hayo ameyasema leo katika shughuli ya mtoto wa Amir maarufu kama "Laca Fasheni" ya kutimiza mwaka mmoja ya mtoto wake ambapo alitumia fursa hiyo kwenda kuwatembelea wagonjwa na kutoa sadaka ya vitu mbalimbali.
Ametoa pongezi kwa familia ya Laca kwa kufanya jambo la kijamii, vijana kushiriki katika maswala ya kijamii, upendo na mshikamano."Nikupongeze sana Amir kwa kuwaza kitu cha tofauti na wanachokifanya jamii kwa kuenzi siku ya kuzaliwa mtoto wako na kuunganisha kwa jamii ambapo ametoa vitu vya kuwasaidia jamii ni kitu kizuri sana"Msaghaa
Amesema kuwa inatakiwa ifanyike kwa kila mmoja na watu wabadili mtindo wa maisha kwa kuwaza vitu tofauti kama alivyofanya Laca.
"Nimpongeze Amiri kwa kazi nzuri anayoifanya na alichokifanya hiki kinaashiria kuwajali wale ambao wahitaji na kutumia vyema nafasi hiyo," MsaghaaKatika kusherehea siku ya kuzaliwa kwa mtoto huyo wametembelea katika hospital ya Sokoine pamoja na Hospital ya Wilaya ya Singida.
Licha ya hayo Msaghaa amewasisitiza vijana kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, pamoja na kumuunga mkono Daktari Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na kuendelea kutoa miradi mbalimbali mkoani Singida na Tanzania kwa ujumla.
Amiri(Laca) amewashukuru wote waliofika leo kuungana naye amewaomba pia kuwajali na kuwafanyia jamii mambo yaliyokuwa mema.Laca ametumja nafasi hiyo kuiomba jamii kuwa kumuabudu Mungu na kufanya toba ya moja kumrudia Mungu.
"Nawashukuru kwa kufika kwenu nawaomba tufanye toba ya kweli na tumrudie Mungu nawashukuru sana,"Laca
Katika msafara huo umetembelewa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi wameshiriki katika jambo kwa kushiriki.Mwisho.

Post a Comment