Wazazi wametakiwa kuwalinda watoto wao pamoja na kuwapatia elimu juu ya kujilinda na kujikinga na ukatili wa kijinsia ili wafikie malengo yao ambayo wamejiwekea katika maisha yao.
Ameyasema hayo leo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida Patrick Kasango akiwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Mko wa Singida Halima Dendego katika kongamano la mwaka lililofanywa na Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii (SMAUJATA) Mkoa wa Singida ambapo lengo la kongamano hilo lililuwa ni utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Patrick Msinda ameomba ushirikiano kwa Mashujaa wote mkoa wa Singida pamoja na wazazi kuwalinda watoto wao.
"Tuendelee kuwalinda watoto wetu pamoja na sisi Mashujaa tuwe na ushirikiano,"Msinda
Kwa upande wa washiriki wa kongamano hilo Groly Makiya ameipongeza SMAUJATA mkoa wa Singida kwa kuendelea kupigania haki kwa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.
"Nichukue fursa hii kuwashukuru SMAUJATA kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya, kwa hakika imeweka alama katika mioyo yetu,"Amesema.
"Hawa ndugu zangu SMAUJATA wanafanyakazi nzuri sana naomba walindwe ili waendelee na kazi zao vizuri,"amesema
Kongamano hilo lilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi akiwemo Diwani wa Mandewa Baraka Hamis na maafisa wengine.
Kataa ukatili wewe ni Shujaa.
No comments: