HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » VIJANA WAPONGEZWA KUSHIRIKI MAFUNZO YA POLISI JAMII

 

 Na Sylvester Richard

Vijana 78 kutoka Kata za Mungaa na Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida wamepongezwa kwa kujitoa kwao  kupata elimu ya Polisi Jamii itakayowasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa Kata zao.


Pongezi hizo zimetolewa Octoba 5, 2024 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi Mrakibu wa Polisi (SP) Paschal N. Kumburu alipokuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Kata ya Makiungu.

Aidha, Kumburu ametumia nafasi hiyo kuwaelimisha washiriki hao wa mafunzo ya Polisi Jamii juu ya ukamataji salama wa watuhumiwa, haki za binadamu, ujasiliamali, utambuzi na ulinzi wa eneo la tukio.


Hata hivyo, mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakaguzi Kata wa Kata mbili ambao ni Andrew Mwashitete ambaye ni Polisi Kata wa Kata ya Makiungu na Mwinyidad Mwinyiheri ambaye ni Polisi Kata wa Kata ya Mungaa .

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply