Na Sylvester Richard
Amesema hayo kwenye hotuba yake aliyoitoa Octoba 15, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika Chuo cha Uhasibu Singida akiwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni ya " *TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA* " Mkoa wa Singida.
Aidha Dendego amesema kuwa maarifa hayo watayapata kwenye shule na vyuo wanavyosomea kupitia walimu wao huku akiwataka kusoma kwa bididii na kuachana na kujihusisha na matumazi dawa za kulevya, ukahaba, ushoga na vitendo vingine ambavyo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.
Akiongelea juu ya vitendo vya ushoga na usagaji, Dendego amekemea vikali vitendo hivyo na kuwataka vijana kutojihusha navyo kwani vinaweza kuliangamiza Taifa " *_Tunawategemea, ninyi ndiyo akinababa, Baba ni kichwa na sisi ni mwili, mkiuacha ubaba wenu mnaangamiza Taifa"*_ amesema Dendego.
Hata hivyo, Dendego amewataka wanafunzi hao kushirikiana vyema na Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia katika kupinga ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini wahusika ambapo watakamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.
Katika hatua nyingine, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuaandaa kampeni hiyo ambayo amesema itakuwa msaada Mkubwa katika kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Mayunga Raphael Mayunga amewaelekeza wanafunzi wanaoanza masomo wakiwemo wanafunzi wa kidato cha kwanza , kidato cha Tano na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhakikisha wanayatii makatazo wanayopewa na wazazi/walezi wanapotoka majumbani kwao kwa sababu hao ndiyo wanaojua uchungu wao.
Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wawe na marafiki wenye tabia nzuri kuliko kujiingiza katika urafiki ambao unaweza kuwatumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya, ulevi wa pombe, ukahaba, ushogo na starehe zingine ambazo zinaweza kuwahamisha kimawazo kutoka kusoma hadi kuingia kwenye maisha magumu.
No comments: