Na Amini Nyaungo

Ameyafanya hayo jana tarehe 14,10,2024 ambapo alitoa gari moja aina ya Noa pamoja na Pikipili mbili (BOXER) katika sherehe kubwa ya Wahijiu ambayo huwa inafanyika kila mwaka ikikusanya watu zaidi ya elf tatu wa kabila hilo lililojikita zaidi katika Jimbo la Singida Mashariki katika baadhi ya maeneo kama vile Ikungi, Siuyu, Mungaa, Makiungu pamoja na Njia panda.

"Nimetoa usafiri huu kwa ajili yenu iwasaidie katika mambo mbalimbali ikiwemo misiba pamoja na shughuli za kimila," Mgonto.
Aidha ametumia jukwaa hilo kuwaomba wananchi wakajiandikishe ili wapige kura za serikali za mitaa pamoja na kubakia na amani yao iliyopo katika taifa la Tanzania.

Katika sherehe hiyo pia jana alikabidhi zawadi za washindi wa ligi yake ya Mgonto iloyoanza miezi miwili iliyopita na kutamatika kwa timu ya Itaghata kuchukua kombe kwa kuwafunga Kikio kwa mikwaju ya penati.

Sherehe hiyo iliwaunganisha watu mbalimbali ikiwemo viongozi wa Serikali, chama, Machief pamoja na wananchi.
Mwisho.
Post a Comment