Na Amini Nyaungo
Swali hili hapa
" Mheshimiwa Rais, ningependa kukuuliza kuhusu safari yako ya Urusi iliyopita, ulijisikiaje uliposhikana mkono na mhalifu wa kivita Putin ?
"Nani alikuamuru kwenda huko ili kuliwakilisha Bunge la IPU?
Pamoja na matembezi yako nchini Urusi yameleta nini katika Demokrasia na si propaganda ya Urusi ?
"Unakubali kuwa kuitembelea Urusi kabla ya Ukraine ambaye ni muhanga ilikuwa kosa ?
Na unajutia Hilo ? Ahsante
DKT Tulia ameanza na kuyasema tena yale maswali
Lithuania imeuliza yafuatayo kuwa nani alikupelekea kibali cha kuitembelea Urusi ? Kwanini isiwe Ukraine kwanza?
Barua zilikuwa pande zote ndugu wajumbe.
HAPA SASA ANATOA MAJIBU
"Barua zilitumwa kwa uwazi na zilielezwa, na ukitaka nakala ya hizo barua kwa kuwa sio Siri unaweza kuzichukua.
"Barua za kuzitembele Urusi na Ukraine zilitumwa kwa uwazi.
"Safari yangu ilipaswa kuanza kuitembelea Ukraine .
"Ukraine ilitujibu kuwa siku tuliyopanga kuitembelea Rais Zelesky atakuwa Newe York Marekani kwenye kikao Cha NATO.
" Nakipindi hicho mkutano wa BRICS ilikuwa unafanyika.
Kwahiyo ningeacha kwenda Urusi kwa sababu Ukraine haikuwa tayari kunipokea kutokana na muda ?
Hapana...kwanini ?Kwa sababu IPU inaamini katika mazungunzo ya amani.
"IPU imejikita katika Diplomasia ya Kibunge.
Kwa namna hiyo nilivyofanya kile nilichopaswa kufanya.
Na nilifkoei angalau ningepewa pongezi hata kwa hizo jitihada ndogo nilizofanya.
"Na sio kulaumiwa kwa mambo ambayo sijafanya.
Unaniuliza ni nani aliyenituma kwani ni nani aliyemtuma Rais Mstaafu kuitembelea Kiev ?
Nani alimtuma ?
"Tafadhali inapaswa kufikia hatua ambayo nimejieleza mara nyingi kwenu na kwa kila mtu alietaka kueleweshwa kama unahisia kuhusu kuitembelea Urusi bila ya kwenda Ukraine, nimewaeleza mara nyingi.
"Barua zilitumwa kote, nisinge ahirisha safari ya Urusi eti kwa sababu nimeshindwa kufika kwanza Ukraine.
Huku niuliza swali Hilo nilipoitembelea Israel...he Uliuliza ?
Hauku niuliza swali nilipoitembelea Palestine Uliuliza?
Hauniulizi swali kama Hilo nilipoitembelea Sudan.
Hauniulizi swali kama Hilo nilipoitembelea sehemu nyingine.
"Nafikiri acheni tuwe na uaminifu, mna Rais ambaye anapaswa kutenda ndani ya mamlaka yake.
Mmemchagua Rais ambaye anapaswa kutenda ndani ya mamlaka yake.
Ambapo si sawa kwa mtu yoyote
Maswali ambayo mmeuliza nimeyajibu kwa kadri ya uwezo wangu.
"Kulingana na malengo yangu kutokana na suala hili nzima.
Na mnapaswa kujua kuwa nisingeomba kumtembelea Putin kwanza kama isingekuwa Ukraine.
"Na hiyo si sehemu ya kwanza nimeitembelea.
Kwanini inaonekana Mimi kukutana na Putin hivyo ghafla Rais wa IPU nimegeuk tishio ?
"Tafadhali heshimu utu wangu kama ninavyo watendea utu wenu.
"Muda wote nitaendeleza Diplomasia ya Kibunge.
Muda wote nitaheshimu misingi ya IPU lakini pia nawaomba Wanachama wote kukubaliana na misingi ya IPU.
Mimi sio, Mungu Wala sio Malaika, Mimi ni binadam tu, na ninafanya kilichopo ndani ya mamlaka yangu.
"Na nimekuwa nikirudia kueleza juu la suala hili.
"Niliombwa na Task force kufanya kile nilichofanya
Kipi kibaya nilichofanya, kwahiyo nilipaswa kufunga mikono yangu ba kusema haikuwa na tunalopaswa kufanya Kama IPU?
"Isingekuwa sawa kwa mamlaka mliyonipa ,nipeni nafasi ya kuiongoza hii taasis kwa mujih wa misingi tunayoisimamia.
Na sio kunilaumu kwa sababuvnatokea nchi flan.
Baashi yenu mnaweza kudhani bado tunatawaliwa kiakiliv, hapana. Hapa hatutawaliwi.
"Hivyo tafadhali acheni tuheshimiane nafanya kadri ninavyowezavnq hivyo ndogyo nitakavyofanya.
Hilo ndilo jukumu langu kwenu na nitaendelea kufanya hivyo ahsante sana
DKT TULIA ACKSON pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini pamoja pia ni Speaker wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
No comments: