HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » DENDEGO KUWALETA WANAWAKE ELFU TATU, MAKINDA NDANI MSAGA SUMU KUNOGESHA

 Na Amini Nyaungo

KILA Mkoa unakuwa na aina yake ya kuyaendea matukio muhimu ya kitaifa au ya Kimkoa, lakini Mkuu wa Mkoa wa Singida  Halima Dendego yeye amekuja na aina yake kuweza kuyaendea  matukio ya namna hiyo.
Kwanini ? Mifano ipo mingi sana kuna tamasha kubwa lilifanyika Mkoa wa Singida kama sio mwezi mmoja uliopita basi wiki tatu la Program ya Uwezeshaji ambalo lilifanyika Singida na limefunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Wiliam Lukuvi na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dotto Biteko.
Kwa wale waliokuwa wanamfuatilia Dendego walimuona namna ambayo haja lala katika tamasha lile na hatimaye tumeona lilivyokua zuri.

Siku ya leo tarehe 07.10.2024 Dendego amerudi tena na ubunifu mkubwa ikiwa yeye ndiye kiongozi wa Mkoa akaona elimu ya kupiga kura itoelewe kwa aina tofauti na amejua wazi wanawake ndio hasa wapiga kura haoa nchini kwetu Tanzania.

Ameongea na Waandishi wa Habari na kutoa taarifa juu ya tamasha kubwa na aina ile ile ya kugusa pale pale katika mshono au lugha sahihi ubunifu katika kuyaendea mambo makubwa ya kitaifa, katika taarifa yake leo tarehe 07.10.2024 Dendego amesema ya kuwa  tarehe 10,10,2024 kutakuwa na Tamasha kubwa lililopewa jina la  ‘Wanawake na Uchaguzi wa Serikali za mitaa’ litafanyika viwanja vya Bombadia mkoani hapa.
Dendego akaona kuwa mambo yasiwe magumu sana licha ya taarifa fupi zitatolewa pamoja na elimu ya mpiga kura lakini kutakuwa na wasanii kunogesha tamasha hilo baada ya taarifa.

 

“Tamasha hilo litaambatana na kutoa taarifa pamoja na burudani zitakuwa nyingi  atakuwepo Msaga Sumu,Isha Mashauzi na Anjela Bono pamoja na washerehesaji mahiri kutoka Singida,” amesema

Angalia ubunifu pamoja na akili nyingi aliyoitumia , maneno mengine aliyoyaongea Dendego baada ya dhamira yake ya kutaka kuwafikia watu ambao hawafikiki kirahisi maneno yake haya hapa chini.

 

Tamasha hilo moja ya mikakati ya mkoa  ili kuwafikia Wananchi wengi zaidi hasa wanawake vijana na wenye mahitaji maalumu.

 

 “Ili kulifikia kundi hilo kubwa lazima kuwe na mipango madhubuti ya kuwafikia na kutoa elimu, ili wananchi wafike na watumie haki yao ya msingi ya kupiga kura,” amesema

 

Lakini pia kutakuwa na Mgeni rasmi ambaye ni Anne Makinda Spika wa Bunge Mstaafu pamoja na Kamisaa wa Sensa nchini.

Akaendelea kutanabaisha kuwa endapo watu watakuja  watapata ladha halisi ya mwanamke  na uongozi.

Kwa makadirio yaliyo wazi amesema kuwa Tamasha hilo litahusisha wanawake takribani elfu tatu(3,000) kutoka katika wilaya zote tano za mkoa wa Singida.

 

Lengo lake litabakia  hilo la  kuwahamasisha kuwahabarisha ili washiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

 

Kwa matazamio Watu wazima takribani milioni moja na ziada wanatarajia kushiriki uchaguzi kupiga kura.

 

Sensa ya mwaka 2022 Singida ina watu milioni 2  elfu nane na hamsini na nne.

Dendego atabaki kuwa moja ya wakuu wa miko wenye dira na maono ya wapiga kura wake na kutaka wafike ili wapige kura.

Lakini pia anajua wazi kuna fursa nyingi zitapatikana wote watakaokuja katika tamasha hili kwani watatengeneza mahusiano ya kibiashara hata yale mengi kila kitu kina mwanzo wake.

Sasa unaweza ukajiuliza mbona wanawake tupu vipi wanaume ? nyie pia mnakaribishwa kufika,  sababu ya kupewa jina  la wanawake kutokana na upatikanaji wao lakini hata wanaume njooni.

Elimu zitatolewa lakini sio elimu itakuwa siku ya mtoko pia kwa ajili ya kukutana na watu mbalimbali ambao huenda baadae mkatengeneza fursa za kimaendeleo.

Hapa ningekuwa na vijana wenzangu ningesema Dendego mitano tena kwa bahati mbaya mie sipo hata Ikulu kumshauri Rais basi itabakia kama ilivyo ila huyu 'Maza' anapiga kazi sana na anauwezea Mkao wa Singida.

 

MAONI YA MWANDISHI

Mikoa ambayo inaendelea inatakiwa iwe na ubunifu sana ili kuwavuta watu katika mambo mbalimbali.

Hata katika fursa unaweza ukaisema na kuitangaza  wanaweza wasiifuate lakini kama ukiweka mkazo pamoja na kuwa wabunifu basi utawapata watu na lengo litatimia.

Hili la kupiga kura sio la Dendego bali hili la Watanzania wote katika kufuata haki zao za msingi za kupiga kura.

Dendego yeye ni Mkuu wa Mkoa wa 22 tangu kuanzishwa kwake miaka 60 iliyopita kila kiongozi anakuja na ubunifu wake, ni kweli hajamaliza mwaka lakini anaendelea kuongoza vyema mkoa wa Singida kwa ubunifu wake na anajua fika kuwa bila ya ubunifu mkoa kama huu hauwezi kuendelea.

Vitu ambayo anavifanya na vinanifanya nihisi mkoa utaendelea mosi, yupo vizuri na muda akisema kikao saa tano ujue muda huo kashafika ni nadra sana hasa ukiwa katika mkoa ya watu wavivu.

 

Pili hataki kukaa ofisini anatembelea sehemu mbalimbali kukagua miradi ya maendeleo huu tunaita uzalendo kongole kwake “Mama mdogo” hili jina alijita wakati amefika nimie nimechomkea hapo lakini kazi nzuri inafanyika.

Dendego pia anashirikiana vizuri na viongozi wake na kila mtu amempa uhuru wa kuwa wabunifu katika mipango yao ya sehemu ambazo wamekabidhiwa.

Anayo mengi sana ni mtu anayependa maridhiano pia anafanya mambo  kwa wakati sio kwa mihemko.

Kama tungekuwa Mtwara tungesema Singida kuchele ila kwakuwa tupo Singida basi tuseme Singida Guntoo utakuwa umeitikia Gunto.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply