HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » MAENDELEO HAYAWEZI KUWEPO PASIPO NA USALAMA


 Na Sylvester Richard

Kamanda wapolisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale amesema kuwa wananchi hawawezi kujiletea maendeleo bila usalama wa kutosha katika maeneo yao. 


Amebainisha hayo katika hotuba yake aliyoitoa Octoba 10, 2024 katika  Kijiji na Kata ya Makiungu, Tarafa ya Mungaa alipokuwa akifunga mafunzo ya Polisi Jamii kwa vijana 77 kutoka Kata 2 za Makiungu na Mungaa.


Aidha Kakwale amewapongeza vijana walioshiriki  mafunzo hayo na kuwata kwenda kuwa mfano kwa kuhakikisha maeneo ya Kata zao yako salama kwa kufanya doria na ukamataji salama wa watuhumiwa kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi na kuwapongeza Polisi Kata wa Kata zote mbili ambao ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP.) Andrew Mwashitete Polisi Kata wa Kata ya Makiungu na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSIP.) Mwinyidad Mwinyiheri ambaye ni Polisi Kata wa Kata ya Mungaa kwa kufanikisha mafunzo hayo.


Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi kwenda kujiandikishwa kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi November 2024.


Halikadhalika, Kakwale amewatia hamasa wananchi wanaomiliki silaha (bunduki) isivyo halali kusalimisha silaha hizo kwa hiari kuliko kusubiri kutafutwa.


Akitoa salamu za Kijiji cha Makiungu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Hamisi Haji amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutoa mafunzo hayo kwa vijana jambo ambalo amelitaja kuwa litakwenda kuimarisha usalama wa maeneo wanayotoka. Amewapongeza pia vijana washiriki wa mafunzo kwa kujitoa kwao na kupata mafunzo na kuwasihi kwenda kuimarisha ulinzi na usalama kwa kutumia elimu waliyoipata.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply