Na Amini Nyaungo
MKUU wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amesema kuwa watu wote wanaomtukana Rais Samia mitandaoni wamekula hasara kwani kazi anayoifanya ndiyo inayoongea.Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatuma Mganga, amesema kongamano hili ni kwa ajili ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Amesema uwakilishi wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi katika mkoa ww Singida ni mdogo sana mfano katika vitongoji 2000 vilivyopo mkoani Singida uwakilishi wa wanawake kwenye uongozi ni asilimia 4 tu.Dk.Mganga amesema katika vijiji 441 vilivyopo Mkoa wa Singida ni wanawake watano tu ndo walipata nafasi ya uongozi kuwa wenyeviti wa vijiji ambao ni sawa na asilimia moja tu wakati katika kata 136 ni kata nne tu ndo waliokwenda kuchukua kata.
"Katika Manispaa ya Singida kuna mitaa 53 lakini wanawake waliodhubutu kuchukua fomu na kushinda ni watatu tu wakati katika nafasi ya ujumbe kati ya nafasi 11,000 za wajumbe wa serikali za mitaa wanawake 3,125 ndo wajumbe wa serikali za mitaa," alisema.
Mwisho


Post a Comment