TAARIFA YA SHEIKH ZUBERI HAKUTEKWA

 .

Na Mwandishi Wetu



Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifaa ya matukio mbalimbali yalitokea moja ya taarifa hiyo ni kutoka mkoani Singida ambapo Sheikh ZUBERI NKOKOO kutoonekana taarifa Zaidi ya tukio hilo inasema kuwa ametengeneza ionekane ametekwa kwakuwa alikuwa anadiiwa madeni.

KWA TAARIFA ZAIDI HII HAPA KUTOKA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU DODOMA

Miongoni mwa matukio hayo ambayo yamethibitishwa kwa sababu hizo ni pamoja na tukio la hivi karibuni lililomhusisha Shekhe Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation iliyopo mkoani Singida ambayo pia inajishughulisha na Miongoni mwa matukio hayo ambayo yamethibitishwa kwa sababu hizo ni pamoja na tukio la hivi karibuni lililomhusisha Shekhe Zuberi Said Nkokoo (53) mwalimu wa dini na kiongozi katika taasisi ya Islam Foundation iliyopo mkoani Singida ambayo pia inajishughulisha na Anwani ya Simu: “MKUU POLISI” Simu Namba: 026 2323585 Fax: 026 2323586 E – Mail: info.phq@tpf.go.tz Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, 4 Mtaa wa Posta, S. L. P. 961, 40483 DODOMA 2 shughuli za kuchinja wanyama.

Katika tukio hilo kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kulisambaa taarifa za kutekwa kwa Shekhe huyo na watu aliowataja kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi tarehe 02/06/2025 saa tano usiku akiwa na kiasi cha fedha taslimu shilingi za kitanzania milioni arobaini na mbili (Tshs. 42,000,000/=).Taarifa ya kupotea kwake pia iliripotiwa Polisi.

Baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa Shekhe Zuberi Said Nkokoo hakuwa ametekwa bali alitengeneza tukio la uongo la kutekwa ili kukimbia madeni aliyokuwa akidaiwa na watumbalimbali (majina yao yamehifadhiwa) yenye jumla ya shilingi za kitanzania milioni mia tano ishirini na moja na laki tano (Tshs. 521,500,000/=). Shekhe Zuberi atafikishwa Mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

KUHUSU KUPOTEA AU KUTOONEKANA KWA WATU MBALIMBALI NCHINI

Kumekuwepo na kuripotiwa kwa taarifa katika vituo vya Polisi na nyingine katika mitandao

ya kijamii zikijulisha kwamba mtu au watu fulani wamepotea, hawaonekani au

wamekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa askari wa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi linapopokea taarifa hizo, huanza uchunguzi kwa kukusanya ushahidi kutoka

vyanzo mbalimbali ili kupata ukweli wa taarifa ya nini kilichotokea kwani hauwezi kusema

moja kwa moja kuwa mtu aliyeripotiwa kupotea, kutekwa, kulazimishwa kupotea au

kuuawa bila ya kumpata anayedaiwa kupotea na ushahidi wa kuthibitisha taarifa hiyo ya

nini kilichomtokea, kama alitendewa uhalifu ni nani wahusika, kulingana na sheria, kanuni

na taratibu.

Vilevile, kwa mujibu wa kifungu cha 117 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 marejeo ya

mwaka 2022 na kifungu cha 161 cha Sheria ya Ndoa Sura ya 29 marejeo ya mwaka 2019,

dhana ya mtu kuchukuliwa kuwa amekufa inapaswa kuthibitishwa na mahakama baada ya

miaka mitano kupita kulingana na vielelezo na ushahidi utakaowasilishwa.

Katika matukio ambayo yameripotiwa katika vituo vya Polisi na uchunguzi wa kina

kufanyika na walioripotiwa kupotea kupatikana wakiwa hai na wengine wakiwa wamekufa,

hadi sasa ushahidi kwa baadhi ya matukio yameonesha sababu zake ni kujiteka, wivu wa

mapenzi, imani za kishirikina, kugombea mali, kulipiza kisasi, kwenda nchi nyingine

kujifunza misimamo mikali na kukimbia mkono wa sheria baada ya kufanya uhalifu

Post a Comment

Previous Post Next Post