Na Sylivester Richard
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale Octoba 10, 2024 alipokuwa akiongea na waandishi wahabari katika Kijiji na Kata ya Makiungu Wilayani Ikungi ambapo amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati Jeshi la Polisi linafanya oparesheni za kubaini kuzuia na kutanzua uhalifu.
Katika hatua nyingine, Kakwale amesema kuwa Jeshi la Polisi Singida linawashikilia watu 4 ambao ni Joackim Michael, (36), Afisa Mtendaji Kijji cha Mhintiri, Emmanuel Dandi, (42), Yona Ramadhani, (40), na Dominiko Stephani, (38) wote askari mgambo na wakazi wa Kijiji cha Mhintiri Ikungi Singida kuhusiana na mauaji ya Frank Joseph Mnyalu, (28), mkulima na mkazi wa Mhintiri aliyefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Ihanja baada ya kushambuliwa ofisini na watuhumiwa hao kwa tuhuma za kufanya fujo.
Omeongeza kuwa, baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wamefikishwa Mahakamani huku kesi zingine zikiendelea kuwa chini ya upelelezi.
Hata hivyo Kakwale ameweka wazi mafanikio ya kesi zililizofikishwa mahakamani na kusema kuwa mwezi Septemba washitakiwa 26 wamehukumiwa vifungo mbalimbali kutokana na makosa ya jinai waliyoyatenda.
Aidha, amekemea na kulaani vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuwataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini kuzuia na kutanzua uhalifu.
No comments: