HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WAKANDARASI WASUMBUFU HAWAFAI KUPEWA TENDA, SAMIA MITANO TENA-IGHONDO


Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo ametoa rai kwa Wakandarasi wababaishaji wajiangalie na fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Ameyasema hayo jana katika mkutano na wananchi wa Kata ya Ngimu Wilaya ya Singida Vijijini wakati wa kupokea ripoti ya fedha za mradi  ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo, amesema ya kuwa tayari shilingi milioni 687 zimekwisha ingia kwenye akaunti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Ngimu. 
Ametahadharisha wakandarasi wababaishaji wasipewe tenda wala nafasi katika ujenzi wa kituo hicho maana watakwamisha ujenzi kwa kuwaibia wananchi na kurudisha nyuma juhudi zake za Kuwaletea wananchi maendeleo.

Katika mkutano huo Ighondo ametumia nafasi hiyo kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia Kwa fedha nyingi za mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Ngimu.

"Namshukuru sana Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha Shilingi Milioni 687 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya ambapo ni muda mrefu tangu wananchi wajitolee nguvu kazi ambapo wakajenga boma lakini halikufanikiwa kukamilika," Amesema
 
"Ni miaka 14 ndugu zangu lakini tangu niingie madarakani nimepambana vya kutosha kila nilipopata fursa nilikisemea kituo hiki sasa kitajengwa kuanzia msingi mpaka kikamilike". Rais Samia ametupatia fedha nyingi jimboni kwenye miradi mingi sana na sisi hatuna deni naye tunamwahidi kumpa mitano tena aendelee kuwaletea wananchi Maendele," Ighondo

Pia amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa yeyote yule atakayehujumu fedha za Mradi huo ili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa jamii kusimama imara kulinda na kutunza Miundombinu yote katika miradi iliyojengwa katika Kata hiyo ikiwemo maji,umeme, Barabara, zahanati na vyumba vya Madarasa shuleni.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Dr. Grace C. Ntogwisangu amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza mapema Mwezi ujao huku akitilia mkazo kwa Wananchi kuchangia nguvu kazi ya  20% ili ujenzi huo ukamilike. Amewataka wasimamie fedha hizo ili ujenzi ukamilike kwa wakati.
Wananchi wa kata ya Ngimu wamemshukuru Ighondo kwa kuwatetea bungeni wamemuomba aendelee na kujituma wao ndio wataamua wakati ukifika.


Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply