HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » MADEREVA WATANO WA MABASI WAFUNGIWA LESINI ZA UDEREVA SINGIDA.

Na Sylvester Richard

Madereva watano wa mabasi ya makampuni tofauti wamefungiwa leseni zao za udereva kwa kipindi cha miezi 3 baada ya  kukamatwa na makosa ya kuendesha mabasi yao mwendokasi usioruhusiwa kisheria ambao ni  zaidi ya Km. 100 kwa saa badala ya Km. 80 kwa saa.

Hayo yamebainishwa na Kamaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Mayunga Raphael Mayunga Septemba 19, 2024 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Kituo  kukuu cha Polisi Singida.

Aidha, Mayunga amewataja madereva hao kuwa ni Emmanuel Gusha ambaye ni dereva wa Kampuni ya mabasi ya KATARAMA, Habiee Neema Sule wa Kampuni ya mabasi ya MWANAKWETU, Emmanuel Wilson Madaha wa Kampuni ya mabasi ya KATARAMA, Emmanuel Laizer Malambala wa Kampuni ya mabasi ya HAPPY NATION, na Jofu Mnison Kanyika wa Kampuni ya mabasi ya FRESTER.

Mayunga amesema, madereva hao wamekamatwa wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida likiwa katika oparesheni za kubaini, kuzuia na kutanzu uhalifu ambazo hufanyika mara kwa mara ambapo kwa kipindi cha miezi miwili ya Julai na Agosti 2024 oparesheni hizo zilifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 137 wa makosa mbalimbali ya jinai ikiwemo watuhumiwa wa mauji, kukutwa dawa za kulevya aina ya bhangi, nyara za Serikali na wizi wa vitu mbalimbali.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply