Na Sylvester Richard
Mayunga Machungwa Mihambo (39), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kisonga, Kata ya Shelui, Wilaya ya Iramba Mkoani amehukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo 3.
Mayunga alitenda kosa hilo Agosti 21, 2024 huko katika Kijiji cha Kisonga Shelui ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Agosti 23, 2024.
Aidha, kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri kujitosheleza, Mahakama ilitoa hukumu hiyo kwa Mshitakiwa mbele ya Mh. Luzango Omero Khamsini Hakimu Mkazi Wilaya ya Iramba.
*Toka Dawati la habari Mkoa wa Singida*
No comments: