HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » KIARATU APOKEA TAARIFA AMSHUKURU SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO



By Amini Nyaungo
Baraza la Madiwani Manispaa ya Singida jana limehitimisha kikao chake  kwa siku tatu ambapo kikoa hicho kilikuwa cha kutoa taarifa  ya mwaka wa fedha ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida inayoanzia Julai 2023 hadi Juni 2024.

Katika kikao hicho ambacho Mwenyekiti wake ni Yagi Kiaratu ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida na Diwani wa kata ya Majengo amesema kuwa Baraza limepokea taarifa  iliyoonyesha mafanikio na changamoto kwa mwaka wa fedha 2023 na 2024 ni muda wa kujitathimini kwa taarifa iliyotolewa ili chama cha Mapinduzi kiweze kufanya vizuri tena katika chaguzi zijazo.

Mstahiki Meya ametumia nafasi hiyo  kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za maendeleo ndani ya Manispaa ya Singida.

Lakini pia Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Lucia Mwiru amewataka Madiwani na viongozi kutengeneza Zahanati ya Kisaki iwe imekamilika ndani ya miezi 3 pamoja na jengo la utawala lililopo Mungu Maji.
"Naagiza Zahanati ya Kisaki ikaamilike lakiji pia jengo la Utawala lililipo Mungu Maji nalo likamile haraka iwezekanavyo ili kila kitu kiende sawa," Mwiru

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Singida Neema Lugha ameomba wataalamu waweze kuonesha utaalamu wao katika shughuli zao ili mipango iende vizuri.
Lakini pia amewataka umoja viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ili chama kizidi kuendelea.

Katika baraza hilo wamefanya uchaguzi wa kumchagua Naibu Mstahiki Meya ambaye ameshinda kwa kura zote 24 za wajumbe wakiokuwepo katika baraza hilo hii imetokana na aliyekuwa awali Geofrey Mdama kumaliza muda wake.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply