HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » DIWANI WA IPEMBE AOMBA SOKO KUU, MWINJORI APAMBANA NA SOKO LA VITUNGUU


Na Amini Nyaungo
Diwani wa kata ya Ipembe iliyopo Manispaa ya Singida Mohamed Omari ameomba kujengwa kwa soko kuu la mmkoa wa Singida kwani lililopo lina muda mrefu hivyo liwekwe katika mpango wa kujengwa kisasa.

Diwani huyo ameyasema hayo leo wakati wa Baraza la Madiwani iliyofanyika katika ukumbi wa Veta mkoani Singida ambapo leo ilikuwa siku ya tatu na ya mwisho.


Amesema kuwa sura ya Singida ni pamoja na soko kuu ambapo wananchi wake wanapata mahitaji maalumu kupitia soko hilo hivyo vi vyema kulijenga kisasa.

"Nawaomba ujenzi wa soko kuu mkoani Singida kwani lililopo lina muda mrefu soko hili ni muhimu sana kwani linalisha wananchi wengi wa Singida,"Amesema

Wakati huo huo diwani wa kata ya Utemini Omari Kawawa Mwinjori yeye ameomba wakati soko la vitunguu linatarajiwa kujengwa basi ikiwapendeza soko hilo liwe katika kata yake kwani sehemu wanayo na tayari wananchi wameanza jitihada za kujenga vyoo kwa ajili ya kuweka soko hilo kwa muda.
"Wananchi wangu wamefanya jitihada za dhati kwa kuanza na ujenzi wa vyoo kwa ajili ya kukaribisha soko hilo.

Baraza la madiwani Manispaa ya Singida limetamatika leo ambapo walikuwa wanatoa taarifa za mwaka wa fedha ulioanzia Juni 2023 hadi Julai 2024, baraza hilo litakuwepo tena baada ya miezi 3.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply