Na Amini Nyaungo
Sipo kwa ajili ya kuliongela zao la alizeti
turudi katika msingi wa kichwa cha habari Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima
Dendego yeye ni wa 22 tangu mkoa huu kuanzishwa yaani yeye ni mkuu wa mkoa wa
22.
Utawajua wote leo kuaniza mwaka wao waliongoza
na mwisho wao kupita Chamber Media na ni vyema ukajua siku nyingine nitakuja na
mafanikio yao na wapi wamefeli ila hii sasa itakuwa habari ya kichunguzi wasije
wakanibana.
1. DATUS NGUA
Singida ilianzishwa tarehe 15, Oktoba 1963 na sasa mkoa huo una miaka 60 ikifika
mwezi wa kumi tarehe kama hiyo mwaka huu wa 2024 itakuwa na miaka 61.
Anayetufungulia dimba leo ni Dantes Ngua yeye ameongoza mwaka mmoja tu mkoa huu ambapo aliongoza kuanzia 1963 hadi 1964.
2. PETER KISUMO
Mheshimiwa peter yeye akaongoza mkoa huo kwa
mwaka mmoja pia kuanzia 1964 hadi 1965.
3. RAJABU SEMVUA
Mzee Rajabu yeye aliongoza kwa miaka minne
kuanzia 1965 hadi 1969 amefungua njia ya kuongoza kwa miaka mingi kuliko wa
kwanza na wa pili.
4. KAPILIMA KAPILIMA
Naye akapata angalau miaka 2 akaongoza kuanzia
1969 hadi 1971 akafanya aliyoyaweza akaondoka.
5. KINGUNGE NGOMBALE MWIRU
Mzee wetu huyu aliongoza kwa mwaka mmoja kuanzia
mwaka 1971 hadi 1972 naye alibahatika kupita Singida.
6. MOSES NNAUYE
Huyu ndio Yule mtoto wake aliyekuwa Waziri wa
Habari Nape Nnauye yeye ameongoza kuanzia mwaka 1972 hadi 1975 akapata miaka
yake mitatu Singida.
7. CHARLES KILEO
Kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1977 Charles
Kileo ameshika hatamu mkoa wa Singida.
8. BRIGADIA SILAS MAYUNGA
Kama ulikuwa hujui makamanda walianzia zamani
kuongoza mikoa yeye akapata namba ya kuongoza mwaka mmoja mkoa wa Singida
kuanzia 1977 hadi 1978.
9. ABDALLAH NUNGU
Nungu alipata miaka 3 kuanzia mwaka 1978 hadi
1981 huyu vita vya IDDI AMIN vimemkuta mkoa wa Singida akiwa mkuu wa mkoa
simaanishi kuwa vita vilikuwa hapa hapana bali wakati vinatokea yeye akiwa mkuu wa mkoa wa Singida kama
ilivyo wakuu wa mikoa wengine ambao walikuwa Tanga au Dar es salaam.
10. KAPTENI PETER KAFANABO
Huyu aliongoza kwa miaka 5 akianzia mwaka 1981
hadi 1986 akiwa mkoa wa Singida.
11. PROFESA JOHN MACHUNDA
Yeye amepata mwaka mmoja wa kuiongoza Singida kuanzia
mwaka 1986 hadi 1987.
12. MEJA JENERALI MWITA MARWA
Naye alipita kwa kuongoza mkoa wa Singida kwa
miaka mitatu kwani aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo kuanzia mwaka 1987 hadi
1990.
13.GALLUS ABEID
Mzee wetu amepata miaka yake mitatu kuanzia
mwaka 1990 hadi 1993 hawa wanaonekana wamekubali Singida wamepata kukaa angalau
miaka miwili na zaidi.
14. ABOUBAKARY MGUMIA
Amepata miaka mine kuanzia mwaka 1993
hadi 1997 akiongoza mji wa Alizeti.
15. COL. ANATOLI TARIMO
Yeye ameanzia mwaka 1997 hadi 1997 hadi mwaka
2002 amekula miaka mitano mkoa wa Singida.
16. HALIMA KASUNGU
Bibi Halima alipata miaka minne pia kuiongoza
Singida kuanzia 2002 hadi 2006 akiwa kwa Wanyaturu na Wanyeramba.
17. DAKTARI PARSEKO KONE
daktari aliweka rekodi kuongoza kwa miaka mingi
mkoa wa Singida ameongoza kwa miaka kumi (10) kuanzia mwaka 2006 hadi 2016,
sijui nani atakuja kuvunja rekodi yake.
18. INJINIA MATHEW MTIGUMWE
Huyu yeye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa
wa Singida mwaka 2016 na akaondoka mwaka huo huo.
19. DAKTARI REHEMA NCHIMBI
Mama yetu ameongoza kuanzia mwaka 2016 hadi
2021 amepata miaka mitano ya kuongoza Singida.
20. DAKTARI BINILITH MAHENGE
Yeye ameongoza kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka
2021 hadi 2022 , wakati naingia mkoa wa
Singida mwaka 2021 ndio nimemkuta Rehema Nchimbi lakini ujio wa Mahenge
yeye nimemuona wakati anakuja na wengine ambao nawataja hapa chini.
21. PETER SERUKAMBA
Serukamba yeye kapata miaka 2 kuanzia mwaka
2022 hadi mwaka 2024 ilitosha kuongoza Singida kwa sasa yupo Iringa.
22. HALIMA DENGEDO
Huyu sasa tunawezakusema kitinda mimba kwa
wakati huu naandika makala hii, yeye ndio kwanza hajamaliza mwaka anaendelea
vizuri sana na kuiongoza Singida.
Dendego hivi karibuni amewataka viongozi wa
mkoa huo kuipaisha Singida kuwa katika mikoa inayofanya vizuri katika uchumi.
Dengedo anaendelea na mipango mizuri ikiwa
hakai ofisini kwakwe anatembelea miradi mbalimbali pamoja na kufanya kaguzi
ambapo kwa maoni ya walio wengi wamemkubali kwa anavyoongoza.
Kitu ambacho hadi sasa mimi nimekipata kwake
huwa anajali sana muda akikuambia anatembelea mradi saa tano basi ujue itakuwa
saa tano kweli.
Hiki kitu viongozi wengi wameshindwa kwendana
na muda anafika kwa wakati na hivi ndivyo inavyotakiwa.
Singida ina utajiri wa kilimo cha Alizeti,
Dengu, Mahindi, Langilanga, Viazi pamoja na Wele vinalimwa sana na kazi kubwa
mkoa huo ni kilimo.
Mkoa wa Singida wenye wakazi milioni mbili na
chngachenga unaendelea kukua siku hadi siku.
Maeneo maarufu ni Singida Mjini, Jineri,
Mandewa, Ubungo, Kindai, Munangi, Mwenge pamoja na KILIMA, lakini pia sehemu
kama vile Ilongero, Mrama, Sekotoure , Mwankoko pamoja na Sepuka, Iramba kuna
Mwanduigembe, lamba, Shelui na sehemu nyingine.
Singida ina vyuo vya VETA viwili vikubwa
ikiwemo Singida Mjini na Ikungi na ina vyuo vikuu kama vile T.I.A ,Chuo cha
Maji pamoja na Utumishi.
Singida ina makabila makuu mawili Wanyeramba
pamoja na Wanyaturu ambao kiuhalisia watani wa jadi.
Kuna mabwawa makubwa wenyewe wanaita maziwa
KINDAI pamoja na SINGIDANI lakini mkoa huu una mabwawa mengi mno kama umetembea
sehemu kubwa ya mkoa huu.
Uchumi wao mkubwa na biashara yao ipo Singida
mjini ikiwa katika soko kuu kuna kila bidhaa na soko la Vitunguu na stend ya
magari Misuna hapo kila gari la mkoa wowote unalipata mtu maarufu hapo ni DAFI
NYANDEKWA.
Katika michezo SINGIDA inafanya vizuri
ikiongozwa na Hamis Kitila Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa
Singida (SIREFA) ina timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Singida Black
Stars zipo akademi mbalimbali ina uwanja wa LITI wenye hadhi ya kuchezewa ligi
kuu TANZANIA.
Ikumbukwe Waziri wa Fedha anatoka mkoa wa
Singida Iramba Mwigulu Nchemba.
Kwahiyo Singida imejaa kila utakacho atakaye
aje kwani pia kuna warembo mkitaka kuoa basi njooni Singida watoto weupe warefu
na wanasifa zote wanaume tunazotaka.
Asili ya Singida ni ISINGIDA hili tutakuja
kukuletea kupitia hapa historia ya LITI hadi kufikia leo.
No comments: