Na Amini Nyaungo
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unaenda kufanyika Novemba 27 mwaka huu unasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndio maana hawaandikishi katika zoezi la daftari la mpiga kura kwa mwaka 2025 ambapo uchaguzi mkuu wa wabunge, Madiwani na Rais unasimamiwa na Tume huru ya uchaguzi (INEC) ambao wanautaratibu waokatika usimamizi wa chaguzi mbalimbali.
Hayo ameyasema leo Meshack Philip Mgovano-Afisa Uchaguzi Manispaa ya Singida alipokuwa akiongea na Standard Radio katikaa kipindi cha Zinduka ambapo amesema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utasimamiwa Ofisi ya Rais Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na (TAMISEMI) na utakuwa tofauti na ule uchaguzi mkuu wa mwakani.
Angalia video hii hapo chini wakati akitoa majibu baada ya swali la Amini Nyaungo akiuliza utofauti kati ya uchaguzi mkuu na huu kwanini hawa wa serikali za mitaa hawaandikishwi katika daftari la kudumu la mpira kura.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika Novemba 27 mwaka huu katika mitaa yote hapa nchini.
Mwisho.
No comments: