HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » DENDEGO ATOA RAMANI KUIKABILI HOMA YA NYANI (MPOX),MGANGA AAGIZA


Na Amini Nyaungo

Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego ameweka wazi namna ya kukabiliana na virusi hatari vya homa ya nyani maarufu kama (MPOX) kwa kusema kuwa elimu mbalimbali zitolewe kupitia Radio na Televisheni juu ya hatari ya virusi hivyo.

Dendego ameyasema hayo leo ofisini kwake akiwa na wadau wa afya juu ya kuwakumbusha wananchi kufuata utaratibu uliokuwa bora ikiwa na kujihadhari kwani ugonjwa huo bado hauna dawa au matibabu ya uhakika.

Aidha ameweka wazi kuwa mkoa wa Singida umeweka mikakati ya utoaji wa elimu kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari(Radio, TV) , katika nyumba za Ibada hadi katika mikusanyiko ya watu lengo ikiwa kuwaelewesha wananchi juu ya ugonjwa huu pamoja na namna ya kujikinga.

" Tuwekeze nguvu kubwa katika kujikinga na ugonjwa huu tuwafikie watu wengi kwa wakati mmoja, tutumie Radio na Televisheni kutoa mafunzo mbalimbali," Dendego.

Wakati huo huo wananchi wamehimizwa kujenga utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara ili kuepuka hatari ya kupata maradhi mbalimbali

Katika hatua nyingine Dendego ameonyesha kutoridhisha na hali ya unawaji wa mikono huku akifafanua kuwa Singida kitakwimu haifanyi vizuri katika eneo hilo hivyo wanapaswa kujitahidi kutunza afya zao kwa kunawa mara kwa mara.

Naye Katibu tawala mkoa wa singida Daktari Fatuma Mganga ameagiza vifaa vilivyokuwa vinatumika kunawia mikono wakati wa Covidi vikatumie ili kujilinda na ugonjwa huo.

Huku Mganga mkuu wa mkoa wa Singida amesema Mkoa unaendelea kuchukua tahadhari na kupanga mikakati mbalimbali inayolenga kuzuia ugonjwa huo kila mmoja anapaswa kuyafuata ili kujizuia yeye na familia yake na watu wanaomzunguka.

Ugonjwa wa Mpox  huambukizwa kutoka kwa  wanyama kwenda kwa binadamu lakini pia  unaambukiza  kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine  kupitia kugusana  na mtu  aliyeambukizwa  au vifaa vilivyotumiwa na mgonjwa kwani maji maji  ya mwili au vidonda vya mtu aliyeathirika  hubeba vimelea  vya Mpox.

mwisho.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply