HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TAKUKURU ZUIENI ILI YAISHE KABLA YA KUPAMBANA-DIGHA


Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Singida Elia Digha ameishauri Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza kitendo cha kuzuia kabla ya kufika katika hatua ya kupambana ili matendo hayo yakome katika hatua ya kwanza kabla ya kufika kwenye kupambana.

Ameyasema hayo jana katika Baraza la Madiwani iliyofanyika Ilongero katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida akiwaomba wasimamie haki ili matendo hayo yaishe na kazi mbalimbali ziendelee.
"TAKUKURU zuieni Rushwa kabla ya kufika hatua ya kupambana, mkifanya hivi mtakuwa mmesaidia miradi ya maendeleo kukamilika kwa wakati na kuondoa viashiria vya Rushwa,"Digha

Wakati huo huo Dighaa ameishauri Serikali kuendelea na mfumo wa "Force Account" wakati wa manunuzi na utekelezaji wa miradi ambayo wanaileta katika halmashuri zao.


"Mie naona ule mfumo wa Force Account unafaa sana uendelee unarahisisha mambo mengi,"Ameongeza.
Katika baraza hilo madiwani wamewasilisha  ripoti zao moja ya taarifa kutoka kata ya Mughunga hakuna mawasiliano ya simu kutoka na mtandao kuwa wa taabu, Digha ameomba taasisi ba Serikali kujenga minara ili nawao wapate mawasiliano.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply