Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Ambwene Kajula amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika mashariki akitokea mkoa wa Singida.
Baada ya kuchukua fomu hiyo Kajula ameweka wazi nia na lengo lake la kugombea nafasi hiyo kuwa kiunganishi kati ya nchi ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki.
“Nimechukua fomu hii ili niwe kiunganishi kizuri Tanzania nan chi za Afrika Mashariki pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali zitakazojitokeza,”Kajula
Kajula anaouzoefu wa sisasa na usimamizi mbalimbali ambao ameupitia katika sehemu alizowahi kuongoza.
Vifuatavyo ni baadhi tu ya vile ambavyo amevisomea ana "Master in Education Management and Planning" ambayo ameipatia katika chuo kikuu cha St Augustine kilichopo jijini Dar es salaam kuanzia mwaka 2019 hadi 2023. Licha ya hayo ana "Post Graduate Diploma in Mass Communicaiton" aliyeipatia chuo kikuu xha Dar es salaam mwaka 2014 had 2017.
Bado anaendelea na elimu Kajula ambapo elimu yake na sekondari aliipatia Siha Kidato cha tano na sita mwaka 1998 hadi 2000 huku kidato cha kwanza hadii cha nne amesoma sekondari ya National Institute of Transport Dar es salaam.
Huku shule ya Msingi ameisomea katika shule ya Msingi Ubungo mwaka 1987 hadi 1993.
Lakini pia ana ujuzi mwingine wa kutumia Compture ambapo ameusoma mwaka 2010 pale British Councel Dar es Salaam.
Kwa upande wa kazi ana uzoefu wa hali ya juu sana ambapo hadi sasa yupo chuo cha Uhasibu tawi la Singida akihudumu kama "Waden" alianza mwaka 2021 hadi sasa.
Aliwahi kuwa sehemu ya kusimamia uchaguzi mkuu wa Tanzania katika mkoa wa Dar es salaam .
Aliwahi kuwa kuwa "Deputy Academic Mistress & Secretary of Quality Assuarance Committee huko Bagamoyo mkoani Pwani.
Aliwahi kufundisha somo la Biology Kwiro Sekondari mkoa wa Morogoro, aliwahi kuwa mhudumu yaani huduma kwa wateja katika mtandao wa simu wa Celtel sasa Airtel mwaka 2006.
Kajula ni shujaa, ni Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania(SMAUJATA) mkoa wa Singida.
Katika nafasi hii anayoigombea aliwahi kuigombeà mwaka 2022 lakini pi nafasi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi.
Kajula ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anashiriki katika shughuli mbalimbali za chama hicho.
Mwisho.
No comments: