Na Amini Nyaungo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TAA Suphian Juma Nkuwi amewatoa hofu Wananchi wa Singida na Watanzania ya kuwa wataendelea na upandaji wa miti mbalimbali ili kuweka rangi ya kijani katika taifa la Tanzania.
Hayo ameyasema leo alipokuwa anafanya mahojiano na Standard Radio katika kipindi cha Zinduka kinachoruka asubuhi saa kumi na mbili na nusu hadi saa nne Jumatatu hadi Ijumaa ambapo mada ilikuwa ikielezea umuhimu a uoandaji wa miti na faida zake kwa jamii.
Suphian amesema kwa mkoa wa Singida watahakikisha ukame hauwezi kuathiri zoezi lao la upandaji miti na watahakikisha watailinda na kuieneza ukijani katika mkoa huo.
Licha ya kuwepo Singida bado wanaendelea kupanda miti mikoa mingine ya Tanzania.
Suphian ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na kuwa mzalendo namba moja katika kampeni yao ya upandaji wa miti.
Wakati huo huo Suphian amejibu maswali ya wasikilizaji walipouliza juu ya maendeleo kufika vijijini na vipi kama unataka Taasisi gau shule yako ipandwe miti, amesema ya kuwa utaribu uliopo kama unahitaji kupanda miti basi uandike barua ukieleza lengo pamoja na kuwa na uhakika wa kuilinda miti hiyo katika ukuaje wake.
Hadi sasa taasisi hii ya TAA imepanda miti sehemu mbalimbali mkoani Singida kwa ajili ya kuiweka salama na kuing'arisha Singida.
Mwisho.
No comments: