HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » SINGIDA KUPINDUA MEZA KIBABE UCHUMI

 Na Amini Nyaungo

Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo ipo nyuma katika uchumi hapa Tanzania, sasa Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego ameweka malengo yake ndani ya mkoa huo ya kuwa unatakiwa kupindua meza iwe katika mikoa ambayo ipo katika tatu bora kiuchumi.

 Dendego amesema anadhamira ya dhati na  kuhakiksiha mkoa huo unaingia katika mikoa mitatu bora yenye uchumi wa uhakika.

Amesema hayo leo wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kinachowashirikisha viongozi mbalimbali wa mkoa wilaya na tarafa.

“ Mipango yetu Singida iwe katika tatu bora ya mikoa ambayo ipo vizuri kiuchumi, tunataka kupindua meza kibabe,” Dendego

Ameongeza kuwa  matarajio na mategemeo yake ni kuona viongozi hao wanakwenda kutoa mchango utakaoleta mabadiliko chanya ndani ya mkoa wa Singida. 

Leo Mkuu huyo wa mkoa amefanya kikao kazi muunganiko wa kikao kazi hicho umejumuisha ngazi zote za maamuzi kuanzia kwa katibu tarafa mpaka ngazi ya mkoa.

Singida ni mkoa ambao upo katikati ya Tanzania na uchumi wake mkubwa unategemea kilimo pamoja na biashara nyingie.

Mazao yanayozaliswha kwa wingi ni pamoja na Vitunguu,Alizeti, Wele,Dengu  Viazi,Langilanga ambao ni mtama pamoja na mahindi .

Mwisho.

 

 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply