Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa Seneti ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM ) mkoa wa Singida Masatu Bure Salum leo amefungua tawi la chama hicho chuo cha VETA Wilaya ya Ikungi na kugawa kadi za chama zaidi ya 100.
Bure amewaambia wanafunzi hao kuwa maendeleo ya nchi hii yanatokana na ustawi bora wa Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake wanaoongoza nchi.
Amewaomba inapofika wakati wa maamuzi basi waangalie viongozi wa CCM ambao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli.
Aidha katika ufunguzi wa tawi hilo amewaomba vijana kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi kama wanaona wanavyo vigezo, ameainisha ya kuwa katika uchaguzi ujao fomu ya Rais ndio pekee itakuwa moja lakini zingine zote zinatakiwa vijana wachukue kwa ajili ha kuomba nafasi mbalimbali.
"Nawasihi mkachukue fomu kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Ubunge pamoja na Diwani sehemu pekee itakayokuwa na fomu moja ni Rais, vijana kachukueni fomu muwanie nafasi mbalimbali," Masatu.
Katika tawi hili Bure ameomba wapatikane viongozi wa tawi ambapo Mwenyekiti, Katibu pamoja na Hamasa wameweza kuchaguliwa baada ya kikao hicho wamepata nafasi ya kushukuru kwa kupewa nafasi hiyo na kuahidi kukuza na kuendeleza mazuri ya Chama cha Mapinduzi.
Mwisho.
No comments: