Na Amini Nyaungo
Uzinduzi huo umefanyika leo baada ya kualikwa na wapenzi wa Simba na kuitikia wito, katika risala yao wamemuomba Mgonto awasajilie tawi hilo na wanahitaji kadi za uanachama ili nawao wajumuike na wenzao.
Mgonto amewakubalia na kuwataka watengeneze mfumo bora wa usafiri ili waje kushuhudia mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba.
"Tengenezeni mfumo mzuri mje Dar es Salaam mshuhudie Simba ikimchapa Yanga katika mechi zao, hili ombi lenu la usajili litakuwa limeisha hadi hapo, " Mgonto
Kuashiria siku maalumu ya Simba , tawi hilo limechinja mnyama Mbuzi kuashiria kuwa Simba anakula Nyama na damu iliyomwagika ishara ya rangi halisi ya Simba.
Wanachama wamefurahi uwepo wake na kuitikia wito kufika na kuzindua tawi lao.
Baada ya kutembelea vijiwe vya kahawa pamoja na sehemu za biasahara na kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa zao mwihso alitamatika kwa kuangalia mpira na mashabiki wa tawi hilo na wengine waliofika katika vibanda umiza.
Simba imefanya tamasha lao leo ikifikia tamasha la 16 tangu kuanzishwa kwake.
No comments: