Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Jesca Kishoa alifanya ziara ya kutembelea wananchi wake katika jimbo la Mkalama ikilenga kutatua kero, kuwajulia hali pamoja na kushiriki shughuli za kijamii.
Ndani ya mwezi wa saba Kishoa alifanya ziara ya kikazi kuanzia tarehe 06.07.2024 katika Kata ya Mwangeza na kutoa mifuko Hamsini (50) ya Saruji na Taa za umeme kwa ajili ya umaliziaji wa Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Mwangeza.
Katika ziara hiyo Mbunge hiyo aligawa mitungi ya Gesi ya kupikia kwa kina mama lishe 56 katika Kata ya Mwangeza sambamba na kumwezesha mtaji Mama mmoja mwenye mahitaji Maalum.
Bila kusahau wanamichezo aligawa jezi seti 18 na mipira 18 katika ziara yake katika kata hiyo ya Mwangeza pamoja na kutembelea familia mbalimbali za wafiwa katika Kata za Mwanga, Matongo na Gumanga ili kuwafariji Kwa misiba iliyojitokeza katika familia hizo za wana Mkalama wenzake.
Mwisho Kishoa alipokea kero mbalimbali za wananchi ambapo baadhi yake amezitatua hapo hapo zile nyingine aliahidi kuzipeleka Serikalini kupitia vikao vya Bunge ili zipatiwe ufumbuzi zaidi.
Kishao ataendelea na Ziara zake za kikazi mwezi huu wa nane zitaendelea Kwa kishindo kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na kero zao kutatuliwa inavyostahiri.
Credit: Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalum- Jesca Kishoa mkoani Singida.
Mwisho.
No comments: