Na Sylvester Richard.
Amebainisha hayo Agosti 1, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida alipokuwa akitoa elimu ihusuyo maswala ya uchaguzi kwa Watendaji wa Kata Wilaya ya Manyoni, Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini na wazee mashuhuri kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2024.
Aidha, Mwakyusa amesema kuwa kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga au kupigiwa kura anao wajibu wa kuzifahamu na kuzifuata sheria, taratibu na miiko ya uchaguzi tangu kuanza kwa mchakato hadi kuapishwa kwa washindi katika uchaguzi huo.
Naye Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Elisante Olomy kutoka Makao Makuu ya Polisi kitengo cha Polisi Jamii, amewataka wanachi wanaotarajia kugombea nyadhifa mbalimbali kutojiingiza katika imani za kishirikina kwa kuamini kuwa watashinda katika nafasi watakazogombea ambapo amewasihi kupiga kampeni, kunadi sera zao na kumwamini Mungu.
No comments: